TANGAZO
TAMASHA LA KUOMBEA AMANI
MKOA WA MTWARA
TUKIWA TUNAELEKEA KWENYE
TUKIO MUHIMU LA UCHAGUZI MKUU KWA MUSTAKABALI WA TAIFA LETU LA TANZANIA,
ASKOFU ANGELUS MCHOMANJOMA
WA KANISA LA SAYUNI INTERNATIONAL PENTEKOSTE LA LUKULEDI-MASASI KWA
KUSHIRIKIANA NA UMOJA WA MAKANISA YA PENTEKOSTE WILAYA YA MASASI MKOANI MTWARA
ANAWATANGAZIA WANANCHI WOTE WA MKOA WA MTWARA NA TANZANIA KWA UJUMLA KUWA
KUTAKUWA NA TAMASHA LA KUOMBEA AMANI SIKU YA TAREHE 11/10/2015.
LENGO LA TAMASHA HILO NI
KUOMBEA AMANI ILI MATOKEO YA UVUNJIFU WA AMANI YASIJITOKEZE KATIKA KATIKA
KIPINDI HIKI CHA KAMPENI NA BAADA YA MATOKEO KUTANGAZWA.
TAMASHA HILO LA KIHISTORIA
KUWAHI KUTOKEA MKOANI MTWARA LITAFANYIKA KWENYE VIWANJA VYA BOMA MJINI MASASI
KUANZIA SAA 8:00 MCHANA HADI SAA 12:30 JIONI.
KWAYA MBALIMBALI
ZITAMWIMBIA NA KUMSIFU BWANA ZIKIONGOZWA NA KWAYA KUTOKA MLINGULA PAMOJA NA
NYINGINEZO NYINGI KUTOKA NDANI NA NJE YA MKOA WA MTWARA.
MAASKOFU,WACHUNGAJI KUTOKA
NDANI NA NJE YA MKOA WA MTWARA WATAHUBIRI NENO LA MUNGU.NJOO USIKIE NAMNA AMANI
INAVYOWEZA KULINDWA HASA KATIKA KIPINDI HIKI CHA UCHAGUZI MKUU.
MGENI RASMI ATAKUWA MKUU WA
WILAYA YA MASASI MHESHIMIWA BERNALD NDUTA.
KAULI MBIU: AMANI, UMOJA NA
MSHIKAMANO NDIO MSINGI MKUU
WAEBRANIA: SURA 12, MSTARI
14….TAFUTENI AMANI KWA WATU WOTE.
EWE MKAZI WA WILAYA YA
MASASI NA MKOA WA MTWARA KWA UJUMLA HII SI YA KUKOSA KWANI NI BUREEEEEE.
WOTE MNAKARIBISHWA!!!!
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD