TANGAZO
Na Hamis
Nasiri,Masasi.
VIJANA
wilayani Masasi mkoani hapa wametoa tamko lao kuwa hawapo
tayari
kuwa sehemu ya machafuko katika uchaguzi mkuu utakaofanyika
Oktoba 25
mwaka huu na badala yake watapiga kura kwa amani na utulivu.
Wito huo
waliutoa jana wilayani humo wakati walipokuwa kwenye jukwaa
la vijana
lenye lengo la kutoa elimu ya utawala bora na haki za kiraia
kwa
vijana na wanawake wilayani Masasi sambamba na kutoa hamasa kwa
vijana
kupiga kura kwa amani,ambapo zaidi ya vijana 100 walishiriki
jukwaa
hilo.
Jukwaa hilo
liliratibiwa na shirika la mtandao wa maendeleo
ya vijana
(MASAYODEN) lililopo Masasi.
Walisema
katika kuelekea uchaguzi mkuuu Oktoba 25 mwaka huu vijana
wilayani
Masasi hawatakuwa mstari wa mbele kushawishiwa na wanasiasa
kuwa
sehemu ya vurugu siku ya uchaguzi na kwamba watakachokifanya ni
kupiga
kura kwa amani na utulivu ili kulinda masilahi ya taifa na
kizazi
kijacho.
Kwa
upande wake Halmada Kalanje alisema vijana ndio msingi wa amani
ndani ya
taifa hivyo wanatambua kuwa kuna maisha baada ya uchaguzi na
kusisitiza
kuwa suala la kutunza amani lipo kwa vijana na kwa kipindi
hiki cha
uchaguzi watahakikisha wanawahamasisha vijana wengine kuwa
siku ya
kupiga kura wapige kura na kuondoka kwenye vituo hivyo vya
upigaji
kura.
Alisema
kauli zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa majukwaani kuwa
wapiga
kura hasa vijana wakimaliza kupiga kura wasiondoke kwenye vituo
vya
kupigia kura ili kulinda kura kauli kama hizo zinaweza kuvuruga
amani
hivyo vijana wanapaswa kuchagua viongozi watakaoliongoza taifa
kwa
usahihi.
Nae
mshiriki mwingine katika jukwaa hilo,Asha Hajiri alisema ni lazima
vijana
wawe kinara katika kuchagua viongozi ambao wanaviashiria vya
kuleta
maendeleo na kubadilisha hali za vijana na taifa kwa ujumla na
kwamba hakuna
sababu ya kuchagua viongozi kwa itikadi za kidini au
kabila.
“Tusikubali
kupiga kura na kukaa katika vituo vya kupigia kura bali
tukipiga
kura tuondoke kwenda majumbani kwetu kusubili matokeo …twende
tukachague
viongozi bora na sio bora kiongozi,”alisema kijana
mwingine
aliyejitambulisha kwa jina la Peter Richard.
Awali
akifungua jukwaa hilo,ofisa mipango wa halmashauri ya mji wa Masasi
Dadi
Shaibu kwa niaba ya mkurugenzi wa halmashauri hiyo aliwaasa
vijana
hao kuhakikisha wanadumisha amani kwa kupiga kura kwa amani na
kuchagua
viongozi watakaowaletea maendeleo.
Alisema
lengo la mradi huo ni kuongeza ushiriki wa vijana na wanawake
katika
mchakato wa uchaguzi wa viongozi ngazi ya kata,jimbo na taifa
kwenye
kuchagua viongozi hao siku ya Oktoba 25 mwaka huu.
Kwa
upande wake katibu wa shirika hilo lisilo la kiserikali wilayani
humo la
MASAYODEN, Salumu Katondo alisema mradi huo wa kuimarisha
utawala
bora na haki za kiraia kwa vijana unatekelezwa na shirika hilo
chini ya
ufadhili wa The foundation for civil Society.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD