TANGAZO
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Mtwara ACP Henry Mwaibambe
Na Fatuma Maumba: Mtwara.
JESHI la Polisi Mkoani Mtwara,limekanusha taarifa iliyotolewa
jana Septemba, 29 mwaka huu majira ya saa 8: 00 mchana kwenye mtandao wa kijamii wa “Jamii
Forum” iliyoandikwa kuwa kituo cha Polisi wilaya ya Masasi mkoani humo
wamekamatwa watuhumiwa wawili wakiwa na masanduku ya kupigia kura na fomu za
kupigia kura zipatazo elfu mbili zikiwa tayari zimetumika na kumpa alama ya
vema mgombea wa Urais kupitia chama cha mapinduzi CCM Mhe. John Pombe Magufuli
na mbunge wa CCM jimbo la Masasi Mwalimu Rashidi Chuachua.
Akizungumza leo na waandishi wa habari ofisini
kwake,Kamanda wa polisi Mkoa wa Mtwara, ACP Henry Mwaibambe, amesema mtandao
huo umeandika kwamba watuhumiwa hao
baada ya kufika kituo cha polisi Mkuu wa wilaya ya Masasi,Bernald Nduta, aliingilia
kati na kulazimisha watuhumiwa hao
waachiwe kwa dhamana kwa amri ya mkuu huyo wa wilaya kitu ambacho si cha ukweli
ni cha upotoshaji.
“Taarifa hizi ni za uongo na hazina chembe yeyote ile ya ukweli…hata mimi nashangaa taarifa hizi
zinatoka wapi taarifa hizi hazina lengo zuri kwa watanzania hususani kwa
wananchi wa mkoa wa Mtwara nahaidi
tutamtafuta kwa juhudi zetu zote huyo
mtu aliyetoa taarifa hizi na kwamba jeshi la polisi linasikitika sana”.alisema
Mwaibambe.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Mtwara amesema hakuna Mtu
wala watu ambao wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani humo kwa kosa la
kukutwa na masanduku ya kura na karatasi za kupigia kura huo ni uzushi na uvumi
tu na kwamba hakuna ukweli wowote lengo
ni kupotosha jamii.
“Ndugu
zangu wanahabari nyinyi ni mashuhuda kuwa hivi karibuni mwenyekiti wa tume ya
Taifa ya uchaguzi Jaji mstaafu Damiani Lubuva alisema mbele ya waandishi wa
habari kuwa masanduku ya kupigia kura kutoka Afrika ya kusni yataanza kuwasili nchini
mwishoni mwa mwezi huu na yatasambazwa mikoani sasa sijui watu hawa wana nia
gani kwa Taifa letu”.alisema Mwaibambe.
Aidha amewaomba wananchi mkoani
Mtwara na Tanzania kwa ujumla kuwa
katika kipindi hiki cha uchaguzi si vizuri kuwapa hofu isiyostahili watanzania,si vizuri kuwapa
watanzania mambo ambayo si ya kweli kwani kwa kufanya hivyo ni kujenga chuki
kwa vyombo vya usalama na tume ya taifa ya uchaguzi ili wananchi waamini kuwa
masanduku ya kupigia kura tayari yapo hapa nchini.
Amesema hadi sasa kampeni za uchaguzi mkoani humo zinaendelea vizuri
licha ya kukiri kuwa ziko baadhi ya changamtoo ambazo amehaidi kuzishughulikia
ikiwemo taarifa za kuwa baadhi ya wagombea kuwaambia wanaume kuwa kama wameoa
basi siku ya kupiga kura wafiche kadi za wake zao ili wasiende kupiga kura
kumchagua kiongozi wanayemtaka.
Kamanda Mwaibambe licha ya kuzungumza na waandishi wa habari pia ametoa waraka wa septemba 30 mwaka huu
kwa waandishi wa habari wenye taarifa ya kukanusha uvumi huo uliowastua
wananchi wa mji wa Masasi na mkoa wa Mtwara kwa ujumla.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD