TANGAZO
PADRE Plasidus Mtunguja (aliyeshika fimbo ya kiaskofu) mara baada ya kutawazwa kuwa Abate wa kwanza mwananchi na ni Abate wa tano tangu shirika la Mtakatifu Benedikto lije eneo la kusini mwa Tanzania takribani miaka 100 iliyopita.
Na Mwandishi wetu:Masasi.
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Songea Mhashamu
Damian Dallu amewataka Watanzania kujituma kufanya kazi ili wapate mahitaji yao
ya lazima badala ya kutegemea misaada toka kwa matajiri.
Wito huo ameutoa wakati anaongoza Ibada ya
Kumtawaza Padre Placidus Mtunguja kuwa Abate wa kwanza Mwananchi kuwaongoza
Watawa wa Shirika la Mtakatifu Benedikto Ndanda, zilizofanyika Wilayani Masasi,mwanzoni mwa juma hili
Ametoa mfano, baada ya vita vya pili
Wajerumani waliamua kufanya kazi kwa bidii na maarifa kiasi kwamba leo hii
Taifa hilo ni miongoni mwa Mataifa
makubwa duniani yaliyo juu kiuchumi,na hivyo kuwahimiza Watanzania kuiga mfano
huo badala ya kuwa Taifa tegemezi hata baada ya kufikisha miaka 50 tangu tupate
Uhuru.
Kwa mujibu wa Kiongozi huyo wa Kanisa,haoni
mantiki ya baadhi ya wanasiasa wanaotafuta kuchaguliwa kwa kuwaahidi Watanzania
kuwapatia huduma bure,kama za afya,elimu na maji;badala ya kuwahimiza wafanye
kazi ili kujiinua kiuchumi.
Abate wa kwanza mwananchi Padre Plasidus Mtunguja (mwenye fimbo katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na maaskofu mbalimbali wa kanisa katoliki kutoka nchini na mataifa ya nje mara baada ya abate huyo kutawazwa.
BAADHI ya mapadre waliohudhuriwa ibada hiyo ya kutawazwa Padre Plasidus Mtunguja kuwa abate wa kwanza mwananchi.
KANISA katoliki parokia ya Ndanda,jimbo la Mtwara.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD