TANGAZO
Na Mwandishi wetu, Mtwara.
Hospitali ya Rufaa ya
Mkoa ya Ligula sasa imeondokana na tatizo la upungufu wa vyandarua lililokuwa
likiikabili kwa nusu ya wagonjwa waliokuwa wakilazwa hospitalini hapo.
Hali hiyo imeisha baada
ya kampuni ya simu ya Tigo nchini kutoa msaada wa vyandarua 1,000 vyenye
thamani ya 15 milioni lengo ikiwa ni kuhakikisha jamii haiendelei kupoteza watu
kwa vifo vitokanavyo na malaria.
Akizungumza Mganga Mkuu
wa mkoa wa Mtwara, Shaibu Maarifa alisema hospitali hiyo imekuwa ikikabiliwa na
uhaba wa vyandarua nusu ya wagonjwa wanaolazwa na kuishukuru kampuni hiyo na
kusema kuwa ujio wa vyandarua hivyo utasaidia kuziba pengo lililokuwepo pamoja
na kubadili vyandarua vilivyokuwa vimechakaa.
“Vyandarua tulivyokuwa
navyo ni vya siku nyingi, hivi tulivyo patiwa na kampuni ya Tigo vitasaidia
kupunguza upungufu wa nusu ya wagonjwa ambao tulikuwa nao kwahiyo utasaidia
hospitali yote kuwa na vyandarua na vile vilivyokuwa vimetoka na kuruhusu mbu
kuingia ndani hawatakuwa na nafasi tena kuuma wagonjwa wetu kama mnavyojua mbu
inaongoza idadi kubwa ya vifo pamoja na kuumwa kwa watoto wadogo na mama
wajawazito,”alisema Dk Maarifa.
Akizungumza Meneja Mauzo
kanda ya Kusini, Lilian Mwalongo alisema kuwa nia na madhumuni ya kampuni mbali
na kuboresha mawasiliano ni kuboresha maisha ya mtanzania kwa kugusa maeneo
muhimu ambayo yanamzunguka kila siku ikiwemo afya na kuwa mpango huo unalenga
kugusha nyanja mbalimbali ikiwemo elimu na uchumi.
“Kampuni ya Tigo Tanzania
ukiacha kati ya madhumuni yake ya kuboresha mawasiliano lengo hasa pia ni
kuboresha maisha ya mtanzania kwa kugusa maeneo mbalimbali yanayomzunguka kila
siku kwa kutazama afya, elimu na uchumi na kwakati huu mkoani Mtwara tumepata
fursa yay a kutoa vyandaria 1,000 vyenye thamani ya 15 milioni,”alisema
Mwalongo.
Aidha alisema kuwa
malaria ni moja kati ya magonjwa makubwa yanayoendelea kusababisha vifo kwa
kasi imekuwa ikishambulia sana watoto na wanawake na kuwataka wananchikutilia
maanani suala la matumizi ya neti.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD