TANGAZO
Na Florence Sanawa, Mtwara
WANANCHI mkoani mtwara wametakiwa kujitokeza katika kambi maalum
ya upasuaji wa mabusha inayoendelea katika Hospitali ya Rufaa Ligula
inayoendeshwa na madaktari bingwa kutoka hospitali ya taifa muhimbili
ikidhaminiwa na kampuni inayotafiti na kuchimba gesi Stat Oil.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo Kaimu Mkuu wa
Mkoa wa Mtwara Johansen Bukwali alisema kuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii
kupitia mpango wa taifa wakudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele
imetoa nafasi ya pekee kwa mkoa wa mtwara ambao ni moja kati ya mikoa ambayo
tatizo hilo bado ni kubwa.
Alisema kuwa serikali imekuwa ikigawa dwa katika ngaz ya jamii
ili kukinga na kutibu magonjwa ya Usubi, Kichocho, Minyoo ya tumbo, Trakoma
(vikope), Matende na Mabusha (Ngirimaji) ambayo yalikuwa hayapewi kipaumbele.
Bukwali alisema kuwa lengo la serikali ni kutekeleza kwa pamoja
udhibiti wa magonjwa haya chini ya mpango kwakuunganisha nguvu kwa kutumia
rasilimali zilezile ili kupunguza gharama za utendaji na kuwafikia wananchi kwa
urahisi.
“Kumekuwa na imani nyingi juu magonjwa haya imani hizo zimekuwa
zikiwaogopesha wagonjwa wanaopata magonjwa hayo jambo husababisha watu wengi
kushindwa kupata kinga na kushindwa kujitokeza pelekeni elimu kwa wengine
mkishapata matibabu” alisema Bukwali
Nae Mkurugenzi wa Idara ya Kinga kutoka Wizara ya Afya na Utawi
wa Jamii Dkt. Neema Rusibamayila alisema kuwa magonjwa yasiyopewa kipaumbele
yamekuwa yakiwapata watu wa rika zote jambo linaloonyesha kuwa maambukizi ni
makubwa.
Alisema kuwa vimelea vya ugonjwa wa mabusha vinauwezo wa kukaa
mwilini kwa mtu kwa muda mrefu bila yeye kujitambua ambapo dalili zake huwa ni
homa za mara kwa mara , kuvimba mitoki, kuumwa kichwa, kuvimba sehemu za siri,
kuvimba miguu au mikono na mabadiliko ya ngozi kwenye mikono na miguu.
“Unajua watu wengi ni waoga tu wanakuwa hawaelewi ndio maana
wanawatisha wenzao juu ya upasuaji wa ugonjwa wa mabusha au ngili maji bila
kujua kuwa wanaweza kufanyiwa upasuaji na wakarudi majumbani kwao” alisema
Rusibamayila.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD