TANGAZO
HABARI LEO
WAKATI joto la uchaguzi mkuu wa Rais,
Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu likizidi
kupanda, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeviagiza vyama vyote vya siasa
vilivyosajiliwa kisheria, kutoendesha kampeni zao katika nyumba za ibada.
Rai hiyo imetolewa na
Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Arusha, Richard Kwitega alipozungumza na waandishi
wa habari jana katika Ofisi ya Tume hiyo mjini hapa. Alivitaka vyama hivyo
kuzingatia maadili kama ilivyokubaliwa na vyama vyote 22 na ambayo viongozi wake
waliridhia na kusaini mbele ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Mbali na nyumba za ibada,
NEC pia imeviagiza vyama hivyo vya siasa, kutoendesha kampeni zao katika
taasisi za umma kama vile vyuo vikuu. Kwitega alisema NEC ni chombo huru,
ambacho hakifungamani na chama chochote cha siasa na kwamba jukumu lake ni
kusimamia kwa uadilifu wa hali ya juu masuala ya Sheria za Uchaguzi nchini.
HABARI LEO
SASA ni dhahiri kuwa
kumkaribisha na kuteuliwa kwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kuwa
Mgombea Urais wa Umoja unaoundwa na vyama vinne vya upinzani (Ukawa), umeleta
mgawanyiko ambao umemlazimu Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba (63),
kujiuzulu wadhifa huo.
“Nimeamua kwa ridhaa yangu kuachia
madaraka rasmi ndani ya CUF, nitabaki mwanachama wa kawaida, dhamira yangu
inanisuta. Tumechukua watu waliotoka CCM ambao waliipinga Rasimu ya Katiba
iliyopendekezwa na Jaji Warioba,” Profesa Lipumba aliwaambia waandishi wa
habari katika mkutano aliouitisha.
“Sijashawishiwa na mtu wala
kikundi, ni dhamira yangu inanisuta, mimi ndiye mwanzilishi wa Ukawa, sasa
tumewapokea wanasiasa waliotoka CCM, tumeshindwa kuenzi na kuzingatia maamuzi
yetu kwenye vikao vya Ukawa,” aliongeza.
Alisema ameamua kujiuzulu
kwa sababu ya mambo makuu mawili; moja ni Ukawa kukubali kupokea waliotoka CCM
ambao walikuwa kikwazo kwenye Bunge la Katiba, na pili ni CUF kutothamini
mchango wake na hivyo kuonekana yeye ni kikwazo. Uamuzi wa Profesa Lipumba
umetegua kitendawili cha siku kadhaa kwa wanachama na viongozi wa CUF kuhusu
taarifa zilizoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari vikisema ameamua kuachana
na wadhifa huo.
MWANANCHI
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba ametangaza
kujiuzulu uenyekiti ndani ya chama hicho.
Akizungumzia sababu za kujiuzulu
kwake, Profesa Lipumba amesema amekerwa na hatua ya Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa) ambao CUF ni chama shiriki kushindwa kusimamia makubaliano
yaliyopelekea kuundwa kwa umoja huo.
Amesema Ukawa ulianzishwa kulinda
maslahi ya wananchi yaliyoainishwa kwenye Katiba iliyowasilishwa kwenye Bunge
Maalumu la Katiba, na kwamba nafsi yake inamsuta hivi sasa kuendelea na uongozi
huku waliokuwa wanaipinga Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba wakikaribishwa
kuwania uongozi wa nchi kupitia umoja huo.
Prof. Lipumba amesema baada ya
kujiuzulu atajikita kufanya shughuli za kitaaluma kwa kujihusisha zaidi na
ushauri wa masuala ya uchumi na maendeleo.
MWANAHALISI
MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof.
Ibrahim Lipumba, ametangaza kung’atuka wazifa wake, kwa kile alichoeleza, “kuwa
kikwazo” katika harakati za kukindoa madarakani Chama Cha Mapinduzi
Amesema,
“Katika hali halisi iliyopo ndani ya uongozi wa chama chetu, mimi naonekana
kikwazo. Naonekana nakwamisha mapambano ya ukombozi. Kwamba siwezi kuwa na
mchango wa maana kama mwenyekiti katika mapambano ya kudai haki sawa kwa wote
katika kipindi hiki.”
Aidha, Prof. Lipumba amesema, ameamua kujiuzulu kwa kuwa baadhi
ya viongozi wenzake ndani ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA),
wamewakaribisha wanachama na viongozi wa CCM waliokuwa mstari wa mbele kupinga Rasimu
ya Pili ya Katiba.
Hata hivyo, Prof. Lipumba alikuwa mmoja wa wenyeviti wanne
wanaounda UKAWA, waliokutana na waandishi wa habari makao makuu ya CUF,
Buguruni, jijini Dar es Salaam na kutangaza kumkaribisha Edward Lowassa ndani
ya vyama vyao.
Wenyeviti wengine walikuwa James Mbatia, NCCR- Mageuzi; Emmanuel
Makaidi, National League Democrat (NLD); na Freeman Mbowe, Chadema.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD