TANGAZO
Rais Jakaya Kikwete akiwa kwenye Viwanja vya Nane Nane Ngongo mkoani Lindi. |
Rais wa Jamhuri ya
muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete
amekiri kuwa licha ya kutoa ahadi yake
wakati analihutubia Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa mara ya
kwanza mwaka 2005 ya kuboresha sekta ya kilimo nchini bado sekta hiyo muhimu
imeendelea kukabiliwa na changamoto
nyingi.
Aliyasema hayo jana
wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya wakulima Nanenane kitaifa
yaliyofanyika kwenye viwanja vya Ngongo manispaa ya Lindi.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili kwenye viwanja vya Nane Nane Ngongo Manispaa ya Lindi ambapo alitumia fursa hiyo kuwaaga rasmi wananchi wa mkoa wa Lindi.
Alisema kilimo cha
Tanzania hakiwezi kupiga hatua endapo serikali haitatilia mkazo sekta hiyo kwa
kuleta mapinduzi ya kweli kwenye kilimo ikiwa ni pamoja na kuachana na matumizi
ya jembe la mkono(Chingondola).
Kikwete alizitaja
changamoto hizo kuwa ni pamoja na matumizi ya mbegu za asili kuliko mbegu
bora,kilimo kinachotegemea mvua pekee,matumizi madogo ya mbolea pamoja na elimu
duni ya wakulima.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD