TANGAZO
kauli hiyo ameitoa leo wilayani Masasi alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari baada ya kutakiwa kutoa ufafanuzi kuhusu idadi ya wagombea waliojitokeza kugombea ndani ya chama chake cha NLD mkoani Mtwara.
Alisema kuanzia sasa chama chake kitangaza rasmi kwa wanachama wake wa mkoa wa Mtwara kuwa chama hicho kinajitoa rasmi kwenye umoja wa katiba ya wananchi Ukawa kwa sababu kimeona kuwa viongozi wa Ukawa mkoani humo wamejawa na mizengwe katika kuendesha shughuli mbalimbali za umoja huo.
Mwenyekiti huyo alisema mfumo wa UKAWA ni kugawana majimbo na si kama uongo unaosambazwa na viongozi wa CHADEMA,NCCR mageuzi na CUF mkoani Mtwara,kuwa wagombea wanaopaswa kugombea nafasi za ubunge kwa majimbo ya Ndanda,Masasi na Lulindi ni wagombea wa vyama hivyo na si wagombea wa NLD kama ilivyokubaliwa kwenye vikao halali vya uongozi wa umoja huo Taifa.
Alisema viongozi wa CHADEMA,NCCR mageuzi na CUF wilayani Masasi wamekuwa wakijifanya kuwa wao ndio wababe wa umoja huo na kwamba kila siku wamekuwa wakitoa taarifa za uzushi kwa wananchi mazingira yaliyopelekea chama chake kuamua kuvunja ukimya kwa waandishi wa habari kuwa chama kilichopewa dhamana ya kusimamisha wagombea katika majimbo hayo ni chama cha NLD pekee.
Mwenyekiti huyo aliwataja wagombea wa chama cha NLD watakaosimama kugombea nafasi za ubunge katika majimbo matatu wilayani Masasi kuwa ni Dkt.Emanuel Makaidi (Masasi),Modesta Makaidi ambaye ni mke wa Emanuel Makaidi(Lulindi) pamoja na Mgombea mmoja aliyemtaja kwa jina moja tu la Profesa Mpelumbe atakayajitosa kwenye jimbo la Ndanda.
Alisema umoja wa katiba ya wananchi ndani ya chama chake hauna manufaa yoyote kwa kuwa tayari chama chake kimejipanga kuhakikisha kinapata ushindi wa kishindo bila hata kuwa ndani ya Ukawa na kwamba hata kiongozi wake wa juu DK. Makaidi analitambua hilo licha ya kuendelea kushiriki katika mikutano ya Ukawa.
Alisema anatoa wito kwa wananchi mkoani humo kuacha kudanganywa na viongozi wa CUF ,Chadema na NCCR mageuzi kwani viongozi wa vyama hivyo hata elimu zao ni za chini ukilinganisha na elimu walizonazo viongozi wa NLD pia anashangazwa kuona viongozi wa vyama hivyo wamekuwa mstari wa mbele kujitokeza kujinadi kuwania majimbo hayo.
“Sisi NLD tunatambua wazi kuwa Ukawa tangu umeanza hasa kwa wilaya ya Masasi viongozi wake wamekuwa wakikihujumu chama chetu na kutangaza kuwa mgombea wetu hana mvuto kwa wananchi kutokana na umri wake kuwa mkubwa licha ya kuwa elimu yake ni ya kutosha sasa hujuma kama hizi hatuzikubali,”alisema mwenyekiti huyo.
Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Jijiji Dar es salaam mwenyekiti wa chama cha NLD Taifa Dkt.Emanuel Makaidi amekiri kuwa ni kweli umoja wa katiba ya wananchi UKAWA kupitia vikao vyake halali wamekubaliana kwamba chama cha NLD kisimamishe wagombea kwenye majimbo matatu ya uchaguzi ikiwemo Ndanda,Lulindi na Masasi.
Alisema kimsingi maamuzi ya ukawa Taifa yako wazi licha ya kushangazwa kwake na baadhi ya wanachama wa chama cha wananchi CUF na CHADEMA kuendelea na kampeni za kuomba ridhaa kwa wananchi wachaguliwe kwenye nafasi hizo za ubunge.
“Ndugu mwandishi nashangazwa na kinachoendelea huko Masasi kwani huku juu tayari tumemaliza na makubaliano tumefikia…lakini cha ajabu nasikia jana kuna mgombea wa CUF Ismail Makombe (Kundambanda) amechukua fomu ya kugombea ubunge jimbo la Masasi kwa madai eti anapendwa sana na wananchi wa jimbo hilo”.alisema Dkt.Makaidi.
Kuhusu kujitoa kwenye UKAWA pia amekana kuwa si kweli na kuendelea kuonesha wasiwasi wake wa utendaji kazi wa mwenyekiti huyo wa mkoa wa Mtwara na kwamba atatoa taarifa rasmi namna alivyolishughulikia suala hilo.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD