TANGAZO
MAELFU YA WAOMBOLEZAJI WAMZIKA ALIYEKUWA MBUNGE WA VITI MAALUMU KUPITIA CHAMA CHA WANANCHI CUF MKOA WA MTWARA.
Marehemu Clara Daniel
Mwatuka alizaliwa Mei 11, 1946 huko katika kijiji cha Miyuyu Wilaya ya Newala
mkoani Mtwara.
Alipata elimu ya Msingi
katika shule ya msingi Newala kati ya
mwaka 1953-1956.Mwaka 1957-1960 aliendelea na masomo katika shule ya msingi ya
wasichana ya mtakatifu Maria huko huko wilayani Newala.
Marehemu alijiunga na elimu
ya sekondari mwaka 1976 na kufanikiwa
kuhitimu mwaka 1979 huko katika shule ya
sekondari Mbinga mkoani Ruvuma.
Mwaka 1989-1990 alisoma
masomo ya sekondari katika shule ya sekondari ya Kitangari iliyopo wilayani
Newala na mwaka 1991-1992 alisoma katika chuo cha ualimu Mtwara na kufanikiwa
kupata ualimu daraja la III A.
Jeneza lililokuwa na mwili wa marehemu mbunge wa viti maalumu kupitia chama cha wananchi CUF mkoa wa Mtwara Clara Daniel Mwatuka.
JENEZA lililokuwa na mwili wa marehemu mbunge wa viti maalumu mkoa wa Mtwara kupitia CUF Clara Mwatuka likishushwa kaburini.
Mwaka 1979 -1993 marehemu
Clara Mwatuka aliajiriwa kama mwalimu katika Halmashauri ya wilaya ya Masasi
mkoani Mtwara na alifanya kazi ya ualimu katika shule mbalimbali za msingi
ikiwemo Ndanda na Nanganga wilayani masasi.
KISIASA
Marehemu alikuwa mwanachama
wa chama cha wananchi CUF kati ya mwaka 1993-2010 na kwamba katika kipindi hiko
aliwahi kuwa mkurugenzi wa idara ya uchaguzi kupitia chama chake wilayani Masasi.
NAIBU spika wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania Job Ndugai wakati akitoa salamu za Bunge kwenye mazishi ya marehemu Clara mwatuka mbunge wa viti maalumu CUF mkoa wa Mtwara hii leo kijijini Nanganga wilayani Masasi.
MKUU wa wilaya ya Masasi Bernald Nduta akizungumza wakati wa mazishi ya aliyekuwa mbunge wa viti maalumu mkoa wa Mtwara kupitia chama cha wananchi CUF.
Mwaka 1997-2010 alikuwa
mjumbe wa Halmashauri kuu ya CUF ambapo mwaka 2010-2015 aliteuliwa kuwa mbunge
wa viti maalumu kupitia chama cha wananchi CUF mkoa wa Mtwara.
Akiwa bungeni amewahi kuwa
mjumbe kwenye kamati ya kudumu ya miundombinu.
Marehemu alifariki Agosti 9,
2015 kwa ajali ya gari huko katika milima ya Miyuyu wilayani Newala.
Marehemu ameacha Mume,watoto
na wajukuu.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD