TANGAZO
Na Clarence Chilumba, Masasi.
KUNDI la vijana zaidi ya sita
ambao wanadaiwa kuwa ni wahuni wakiwa na marungu,fimbo,mashine ya kukatia miti
ya mbao (Chainsow) pamoja na mawe wamewavamia wanafunzi pamoja na walimu wa
shule ya sekondari ya kutwa Masasi na kutembeza kipigo shule hapo.
Tukio hilo la ajabu lililovutia
hisia na majirani wa shule hiyo lilitokea jana shuleni hapo majira ya 8:00 mchana
wakati wanafunzi hao pamoja na walimu wakiwa madarasani wakiendelea na masomo.
Akizungumza na waandishi wa
habari shuleni hapo kuhusu kutokea kwa tukio hilo ambalo limeacha gumzo kubwa
wilayani Masasi kaimu mkuu wa shule hiyo Farida Mmuna alisema wakati akiwa ofisini
kwake shuleni hapo majira ya saa 8:00 mchana alisikia wanafunzi wakipiga mayowe
ya kuomba msaada.
Alisema vijana hao zaidi ya sita
wakiwa wamebeba marungu,fimbo,mashine za chainsow na mawe makubwa walivamia shuleni hapo ghafla na kuingia kila
darasa kwa madai kuwa wanamsaka mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo ambaye
anajulikana kwa jina la Shafii Stamili (JEMBE) ambae anasoma kidato cha tatu
ili walipwe fedha yao wanayomdai baada ya kukopa viatu.
Mmuna alisema vijana hao wanamdai mwanafunzi huyo fedha yao
ambayo inatokana na deni la viatu alivyokuwa amekopa kwa vijana hao ambapo
fedha hiyo inadaiwa kuwa ni Sh.15, 000 na kwamba deni hilo ni la muda
mrefu ambapo mwanafunzi huyo amekataa kulilipa.
Alisema baada ya mapigano hayo
baina ya vijana hao, walimu na wanafunzi walimu walifanikiwa kmdhibiti kijana
mmoja miongoni mwa vijana hao na kumuweka chini ya ulinzi huku mwalimu mmoja wa
shule hiyo akiumizwa vibaya mkononi wakati akiwa katika harakati za kuwadhibiti
vijana hao.
“Ghafla hawa vijana walivamia
madarasa yetu na kuanza kuwapiga wanafunzi na walimu wakidai wanahitaji kulipwa
fedha yao kutoka kwa mmoja wa wanafunzi ambaye wanamdai kwa muda mrefu sasa
baada ya mwanafunzi huyo kukopa viatu”.alisema Mmuna
Alisema baada ya wahuni
hao kuona kuwa wamezidiwa nguvu walikimbia
lakini mmoja wao walifakiwa kumdhibiti na kupiga simu polisi ambapo jeshi la
polisi wilayani lilifika na kumtia nguvuni kijana huyo ambapo kwa sasa
anashikiliwa na jeshi hilo kwa mahojiano zaidi.
Akizungumza kwa niaba ya
wanafunzi wenzake mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule hiyo, Ferdinand
Lucas alisema kwa sasa hali ya usalama wao dhidi ya vijana hao uko hatarini na
kwamba wanaiomba serikali wilayani humo kuingilia kati suala hilo ili
kuchunguza kwa undani zaidi.
Nae mwanafunzi ambaye anadaiwa
kuwa chanzo cha mapigano hayo Shafii Stamili alikanusha kudaiwa na vijana hao
na kwamba hawafahamu na hajawahi kukopa viatu kwa vijana hao zaidi ya kuwafahanu kama ni wahuni tu wa mtaani
kwao anakoishi.
Jeshi la polisi wilayani Masasi
limethibitisha kutokea kwa vurugu hizo baina ya vijana hao walimu pamoja na
wanafunzi na kwamba linamshikilia kijana mmoja ambaye miongoni mwa vijana hao lakini
hata hivyo kijana huyo ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja.
Mwisho
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD