TANGAZO
Mbunge aliyemaliza muda wake jimbo la Ruangwa mkoani Lindi Kasim Majaliwa ambaye jana alitangazwa kuwa ndie mshindi wa kura za maoni jimbo la Ruangwa kwa kupata kura 11988.
MADIWANI
tisa wa Chama Cha Mapinduzi jimbo la Ruangwa mkoani Lindi wameangushwa vibaya
kwenye kura za maoni za ndani za chama hicho kwa madai ya kutotekeleza ipasavyo
ilani ya CCM katika kipindi cha miaka mitano iliyopita kwenye kata zao.
Kata
nne jimboni humo hazikufanya Uchaguzi baada ya wagombea wake kupita bila
kupingwa zikiwemo kata za Nanganga, Chibura, Mandawa pamoja na Chunyu.
Walioangushwa
ni pamoja na aliyekuwa diwani wa kata ya Malolo Mohamed Seiph Mtambo,Fabian
Nguli (Chinongwe),Moses Isdor Mpwapwa (Mbekenyera),Kassim Issa Zuberi
(Namichiga), Mosa na Mohamed Mtejela (Nambilanje).
Wengine
walioangushwa ni Abdallah Hassan Mbila (Chienjere), Bakari Mohamed Malenda (Mbwemkuru),
Beda Faustin Mbila (Mnacho) pamoja na Omari Mohamed Imani (Makanjiro).
Aidha
katika kata ya Ruangwa mjini Issa Njinjo ameibuka Kidedea baada ya kujinyakulia
Kura 251 huku mpinzani wake wa karibu Thomas Damas Kambanga akiambulia kura 162
pekee.
Jimbo
la Ruangwa mkoani Lindi lina kata 22.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD