TANGAZO
JIMBO LA MASASI
KATIBU wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Masasi Mwanamasudi Pazi akitangaza matokeo nje ya Ofisi ya CCM (W) kwa nafasi za Ubunge kwa Jimbo la Masasi,Lulindi na Nanyumbu.Kushoto kwake ni Katibu msaidizi wa CCM Ajali Mpataga na kulia kwake ni Mariam Kasembe na Jerome Bwanausi.
MSHINDI aliyeongoza kwenye nafasi ya Ubunge Jimbo la Masasi Rashid Chuachua akitoa shukrani zake baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo nje ya ofisi ya CCM wilaya ya Masasi jana.
Katika jimbo la Masasi lililokuwa na
wagombea wanane aliyeibuka mshindi ni Mwalimu Rashid Chuachua aliyepata kura
2412,Geofrey Mwambe kura 1787,Magreth Mtaki kura 1386,Regnald Kombania
533,Joshua Nnonjela 441,Edwin Eckon 353,Mike Mande 186 na Cleveland Nkata kura
100.
Rashid Chuachua akiwa amebebwa na mashabiki wake baada ya kutangazwa mshindi wa nafasi ya ubunge jimbo la Masasi.
JIMBO LA NDANDA
Kwa mujibu wa katibu wa CCM wilaya ya Masasi Mwanamasudi Pazi alimtangaza
Mariam Kasembe kuwa mshindi katika jimbo la Ndanda kwa kupata kura 5453, Cesil
Mwambe kura 4951 na Raynald Mrope aliambulia kura 863.
MSHINDI wa nafasi ya Ubunge Jimbo la Ndanda Mariam Kasembe (kulia) akitoa salamu nje ya ofisi za CCM wilaya ya Masasi baada ya Kutangazwa kuwa mshindi anayepiga makofi ni aliyekuwa mpinzani wake wa karibu Cesil Mwambe.
Mgombea aliyeshindwa kwenye nafasi ya ubunge jimbo la Ndanda Cesil Mwambe (kushoto) akipeana mikono na Mshindi wa kura za maoni Mariam Kasembe ikiwa ni ishara ya upendo baada ya kutangazwa kuwa mshindi.
Mgombea aliyeshindwa nafasi ya ubunge jimbo la Ndanda Cesil Mwambe akitoa shukrani zake kwa wanachama wa chama hicho nje ya ofisi ya CCM wilaya ya Masasi.
JIMBO LA LULINDI.
Katika jimbo la Lulindi
aliyeibuka kidedea ni mbunge anayemaliza muda wake Jerome Bwanausi
aliyejinyakulia kura 11745, Sowan Thomas kura 1048 na Enock Halinga alifanikiwa
kupata kura 896.
Mgombea aliyeshinda Jerome Bwanausi akitoa shukrani kwa wanachama wa CCM Jimbo la Lulindi kwa kumchagua tena.
Enock Halinga mgombea aliyeshindwa kura za maoni Jimbo la Lulindi akizungumza nje ya ofisi ya CCM wilaya yaMasasi.
JIMBO LA NANYUMBU.
VIJANA na Watoto Wakishangilia kabla ya matokeo kutoka wilayani Nanyumbu.
katika jimbo la Nanyumbu katibu
wa chama hicho wilayani humo Bakari Nachembe alimtangaza William Dua kuwa
mshindi kwa kupata kura 6165 huku mpinzani wake wa karibu Yahya Mhata akipata
kura 6157.
Mbunge anayemaliza muda wake katika
jimbo la Nanyumbu Dastan Mkapa alishika nafasi ya tatu kwa kupata kura
3945,wengine ni Endrick Napacho kura 2096,Majaribu Lupeto kura 931,Uledi
Mwanache 497 na Hassan Wema aliambulia kura 296 pekee.
Polisi wakiimarisha Ulinzi kabla ya matokeo kutangazwa nje ya ofisi ya CCM wilaya ya Nanyumbu
Polisi Nanyumbu Kabla ya Matokeo Kutangazwa
Mgombea aliyeshinda katika Jimbo la Nanyumbu William Dua akizungumza muda mfupi kabla ya matokeo kutangazwa nje ya ofisi ya CCM wilaya ya Nanyumbu.
Mgombea aliyeshindwa Yahya Ally Mhata akitoka nje ya ofisi ya CCM wilaya ya Nanyumbu kabla ya matokeo kutangazwa.
Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Nanyumbu Dastan Mkapa
Jimbo la Nachingwea waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mathias Chikawe ameangushwa vibaya na Hassan Masala aliyejizolea kura 6494 huku yeye akipata kura 5128.
Wengine ni Amandus Chinguile kura
1274,Issa Mkalinga 466,Alli Nanjundu kura 319,Fadhili Liwaka 1171,Albert Mnali
763,Benito Ng’itu kura 797,Mustapha Malibiche 427,Steven Nyoni 1438 na Grayson
Francis alipata kura 671.
Aliyeibuka Kidedea katika Jimbo la Nachingwea Hassan Masala.
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mathias Chikawe ameangushwa
JIMBO LA RUANGWA
Kwa upande wa jimbo la Ruangwa mkoani
Lindi aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo ambaye ni naibu waziri anayeshughulikia
elimu Kasim Majaliwa amefanikiwa kutetea nafasi hiyo kwa kupata ushindi wa
kishindo wa kura 11988.
Wengine katika jimbo hilo ni pamoja
na aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa Issa Libaba
aliyepata kura 555, mwalimu Mohamedi Namtimba kura 596 huku Kada mwingine wa
chama hicho Bakari Nampenya akiambulia kura 2673.
JIMBO LA MTWARA MJINI
Matokeo ya kura za maoni CCM kwa nafasi ya ubunge jimbo la Mtwara mjini
Salumu Nahodha kura 114 sawa na asilimia 0.95,
Mussa Chimae kura 217 sawa na asilimia 1.87,Said Swala
kura 393 sawa na asilimia 3.39,Hussein kasugulu kura 791 sawa na asilimia 6.83
na Hasnen Murji kura10055 sawa na asilimia 86.60.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD