TANGAZO
BAADHI ya wanafunzi wa Chuo cha Quality Development College wakiwa kwenye maandamano ya siku ya wafanyakazi duniani 2014.
WAHITIMU waliomaliza
masomo ya tasnia ya uandishi wa habari na uhudumu wa afya kwenye chuo cha Quality Develepment
College kilichopo wilayani Masasi mkoani Mtwara wametakiwa kwenda kutumia
taaluma zao kwa bidii na uweledi uliotukuka ili taaluma hizo ziweze kuendelea
kuthaminiwa na jamii.
Rai hiyo ilitolewa juzi
wilayani humo na mkuu wa wilaya ya Masasi,Bernad Nduta alipokuwa akitoa nasaha
zake kwa wahitimu hao kwenye sherehe za mahafali ya kwanza chuoni hapo ambapo
sherehe hizo zilifanyika kwenye viwanja vya chuo hicho wilayani humo.
Nduta alisema wahitimu
hao watambuwe kuwa taaluma walizosomea na kuhitimu ni taalumu nyeti na za
msingi katika kutoa huduma kwa jamii hivyo huko waendako katika kufanya kazi
zao ni lazima wakafanye kazi kwa uweledi na ufanisi uliotukuka ili taaluma hizo
ziendelee kuthaminiwa na kuheshimiwa na jamii.
Kwa upande wake makamu
mkuu wa chuo hicho anayesimamia taaluma,Godfrey Nzoka alisema kuwa wanachuo
waliofanikiwa kuhitimu ni 121 ambapo wavulana ni 31 na
wasichana 90 na kwamba chuo hicho kinapokea wanafunzi kutoka mikoa yote
Tanzania ikiwemo,Lindi,Mtwara,Ruvuma,Tanga,IringaMorogoro,Mwanza,Shinyanga,Pwani,Kilimanjaro,na Zanzibar.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD