TANGAZO
MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Julius Kaondo akisisitiza jambo wakati anazungumza kwenye Mafunzo ya Ushirikiano wa Uboreshaji wa Serikali za Mitaa kati ya Tanzania na Japan kwenye ukumbi wa NAF mkoani Mtwara Hii leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya
Wilaya ya Mtwara Julius Kaondo amewataka Maofisa Habari wa Halmashauri za
Wilaya Kote nchini Kufanya Kazi Zao Kwa Weledi mkubwa Kulingana na Taalumza Zao
kwa Lengo la Kuzitangaza Halmashauri zao ili Kupunguza Malalamiko Kutoka Kwa
Wananchi ambao Kila siku wamekuwa wakilalamika Kwa kutofahamu namna Halmashauri
zao Zinavyoendeshwa.
Ametoa Kauli hiyo leo wakati anawasilisha Mada kwenye Mafunzo ya Ushirikiano wa Uboreshaji wa Serikali za Mitaa Kati ya Tanzania na Japan yanayoendela kwenye ukumbi wa NAF Manispaa ya Mtwara Mikindani.
"Vyombo vya Habari nchini Kila siku zimekuwa vikiripoti taarifa mbaya pekee kwa halmashauri nchini...kitu ambacho si kweli kwamba Halmashauri za Wilaya hazifanyi Mazuri hivyo nawaomba maofisa Habari mfanye kazi kuzitangaza kwa mazuri Halmashauri zenu"Aisema Kaondo.
Mafunzo hayo ya siku nne yameandaliwa na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na kufadhiliwa na serikali ya Japan lengo likiwa ni kuwajengea uwezo watendaji wa serikali za mitaa waweze kufanya kazi kwa kujituma zaidi kama ilivyo kwa nchi mbalimbali duniani Japan ikiwemo.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD