Loading...
ADVERTISE WITH US ON THIS BLOG.CALL +255 714 789 592/ +255 682 997 767/ +255 752 944 022

CHAMA CHA MAPINDUZI JIMBO LA MTWARA MJINI CHAZINDUA KAMPENI ZAKE RASMI

TANGAZO

Chama cha mapinduzi jimbo la Mtwara mjini kimetamba kuwa kitaibuka na  ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu ujao oktoba mwaka huu kwa kuwa bado wananchi jimboni humo wanakiamini kutokana na kusimamia na kutekeleza ilani ya chama hicho.

Kauli hiyo imetolewa jana  na mgombea wa nafasi ya ubunge  jimbo la Mtwara mjini Hasnein Murji wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni  ambapo alisema Kukosekana kwa mgombea ubunge kwa tiketi ya umoja wa katiba ya wananchi UKAWA hadi sasa katika jimbo la Mtwara mjini,kunamuhakikishia ushindi wa kishindo yeye na chama chake.

Alisema bado wananchi wa jimbo la Mtwara wanakiamini chama cha mapinduzi na kwamba   ushindi mkubwa alioupata katika mchakato wa kura za maoni ndani ya chama ni ishara tosha kuwa ataibuka kidedea na kwamba kushindwa kwa vyama hivyo hadi sasa kumsimamisha mgombea atakayeshindana nae ni dhahiri kuwa hakuna mpinzani wa kweli jimboni humo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa wa CCM wilaya ya Mtwara mjini Ally Chinkawene alisema katika  jimbo la Mtwara mjini  chama cha mapinduzi kimesimamisha   wagombea  24 wa nafasi ya za udiwani huku  kati yao 18 wa kata na 6 viti maalumu.

Aidha chama hicho katika jimbo la Mtwara mjini lilitumia nafasi hiyo ya uzinduzi wa kampeni katika kuwatambulisha rasmi wagombea wake kupitia nafasi mbalimbali lengo likiwa ni kuhakikisha chama cha mapinduzi jimboni humo na mkoa wa Mtwara kwa ujumla kikipata ushindi.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mtazamo Mpya | Designed By FAHARI YA TANZANIA
Back To Top