Loading...
ADVERTISE WITH US ON THIS BLOG.CALL +255 714 789 592/ +255 682 997 767/ +255 752 944 022

ALIYESHINDWA KWENYE KURA ZA MAONI CCM JIMBO LA NDANDA ATUA RASMI CHADEMA

TANGAZO
Aliyekuwa Mgombea wa nafasi ya Ubunge kupitia CCM wakati wa Mchakato wa kura za maoni katika Jimbo la Ndanda mkoani Mtwara Cesil David Mwambe hii leo amekihama chama hicho na kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA na hatimaye kutambulishwa rasmi kwa maelfu ya wanachama wa chama hicho kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Ndanda.
Kwenye mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM Cesil Mwambe aliangushwa na Mariam Kasembe aliyepata kura 5453 huku Mwambe akipata kura 4951 na Raynald Mrope aliambulia kura 863.  
 Cesil Mwambe akitoa shukrani zake baada ya kutangazwa kwa matokeo ya kura za maoni wakati wa uchaguzi ndani ya chama cha mapinduzi CCM.

Cesil David Mwambe akipongezana na mgombea wa ubunge Jimbo la Lulindi Jerome Bwanausi nje ya ofisi ya CCM wilaya ya Masasi.

Mshindi kwenye mchakato wa kura za maoni Mariam Kasembe akipeana mikono na aliyekuwa mpinzani wake wa karibu Cesil Mwambe baada ya kutangazwa kwa matokeo ya kura za maoni ambapo kwa sasa Cesil amejiunga na CHADEMA.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mtazamo Mpya | Designed By FAHARI YA TANZANIA
Back To Top