Loading...
ADVERTISE WITH US ON THIS BLOG.CALL +255 714 789 592/ +255 682 997 767/ +255 752 944 022

HALMASHAURI YA MJI WA MASASI YAENDELEA KUTEKELEZA MRADI WA TASAF III KWA JAMII

TANGAZO

Zaidi ya wilaya 45 zimeanza kupatiwa mafunzo kazi kwa wataalamu kutoka halmashauri husika juu ya utekelezaji wa miradi ya kutoa ajira ya muda chini ya mpango wa kunusuru kaya masikini unaotekelezwa na mfuko wa maendeleo ya jamii  TASAF awamu ya tatu nchini.

Katika hotuba yake mkurugenzi mtendaji  wa mfuko wa Tasaf nchini Ladislaus Mwamanga iliyotolewa na mwakilishi wake Alphonce Kyagira  wakati wa ufunguzi wa kikao kazi kilichowakutanisha wataalamu kutoka halmashauri ya wilaya na mji wa masasi mkoani mtwara imeeleza kuwa mpango huo unalenga kuwajengea wawezeshaji ngazi ya wilaya uelewa ili waweze kuziwezesha jamii kuibua miradi itakayowapatia ajira na kujiongezea kipato.
Alisema kufuatia awamu mbili za utekelezaji wa mpango wa Tasaf nchini umeonesha mafanikio makubwa ambapo kupitia mradi wa kunusuru kaya masikini unaoendelea kwa sasa wadau wa maendeleo walioshiriki katika kuchangia na wanaotarajia kuchangia mpango huo wakiwemo benki  ya dunia,shirika la maendeleo la kimataifa la uingereza na lile la Sweden yakiwemo UNDP,UNICEF pamoja na ILO yameonesha kuridhishwa na mafanikio hayo ikiwa ni pamoja na kasi kubwa ya utekelezaji wake.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakurugenzi wa halmashauri za wilaya na mji wa masasi mkoani Mtwara Beatrice Dominick na Fortunatus Kagoro walisema mpango huo umelenga kupunguza changamoto zinazochangia katika kuharibu mazingira,endapo wataalamu hao wataweza kusimamia kikamilifu utekelezaji wa mradi huo.


TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mtazamo Mpya | Designed By FAHARI YA TANZANIA
Back To Top