TANGAZO
Na Hamisi Nasiri,Masasi.
WATENDAJI wa kata na mitaa wilayani
Masasi Mkoani Mtwara wameonywa kutokuwa sehemu ya chanzo cha uvunjifu wa amani
katika uchaguzi mkuu wa Rais,wabunge na madiwani utakaofanyika oktoba 25 mwaka
huu badala yake wametakiwa kudumisha amani na utulivu kwenye maeneo yao ya kazi.
Wito
huo ulitolewa jana wilayani hapa na Inspekta,Samuel Daniel wa kituo cha polisi
wilayani Masasi ambaye pia ni mkaguzi mkuu wa polisi kitengo cha polisi jamii
wilaya ya Masasi wakati alipokuwa akizungumza na watendaji hao kwenye kikao
kazi kilicholenga kuwapatia elimu ya ulinzi shirikishi na uendelevu wa amani
kwenye maeneo yao ya kazi.
Aidha watendaji hao wametakiwa kuwa na takwimu halisi za watu ambao wanamaliza vifungo vyao gerezani wanaoishi katika maeneo ili kukaa nao pamoja na kuwapa elimu itakayowafanya waache kufanya ualifu na wawe raia wema katika kutunza amani na utulivu pia wawe viongozi wa kuwaibua wahusika wa matukio ya uvunjifu wa amani.
Alisema katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu kuna mambo mengi yanayoweza kujitokeza ya uvunjifu wa amani hivyo hatua za kulinda amani zinapawa kuchukuliwa mapema kabla ya matukio hayo kujitokeza na kuathiri mambo ya kimaendeleo.
Alisema wilaya ya Masasi kwa sasa imegubikwa na matukio mbalimbali ya uvunjifu wa amani hasa kwa kundi la vijana ambao wamekuwa hawana kazi maalumu za kujiingizia kipato hivyo wanaamua kukaa vijiweni na kutafuta kipato kwa njia isiyo ya halali,kwa kutambua hilo watendaji wa kata na mitaa wanao jukumu kubwa la kuitisha mikutano itakayojadili masuala ya amani na utulivu kwenye maeneo yao.
Alisema watendaji wa kata na mitaa ni walinzi wa amani kwenye maeneo yao wanaofanyia kazi hivyo hawatakiwi kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani badala yake wanatakiwa kuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu kwa jamii iliyowazunguka juu ya ushiriki katika masuala ya amani na utulivu.
Daniel alisema watendaji hao pia ni lazima waanzishe vikundi vya ulinzi shirikishi kwenye maeneo yao ambayo yatasaidia kutoa taarifa kwa watu ambao wana malengo ya kufanya uhalifu katika kipindi cha uchaguzi ili jeshi la polisi liweze kuwa shughulikia mapema.
“Anzisheni vikundi vya ulinzi shirikishi kwenye mitaa na kata hii itasaidia kuifanya jamii kuweza kushiriki katika matukio ya uvunjifu wa amani na kuweza kuwapata wahalifu kwa uraisi zaidi,”alisema Inspekta Daniel.
Alisema jeshi la polisi wilayani Masasi litaendelea kutoa elimu kwa watendaji hao hasa katika kipindi hiki ambacho taifa linaelekea katika uchaguzi mkuu na kwamba lengo la elimu kwa sasa ni kuhakikisha suala la amani linakuwa endelevu kwenye wilaya hiyo hatimaye kuweza kupunguza lindi la matukio ya uvunjifu wa amani.
Kwa upande wake katibu tawala wilaya ya Masasi,Danford Peter alisema ni vema watendaji hao wa kata na mitaa wakazingatia kanuni za utumishi wa umma katika kutekeleza majukumu yao ya kikazi na kwamba iwapo watakuwa viongozi wenye kutambua umuhimu wa amani na utulivu basi hata jamii wanayoiongoza italipa kipaombele suala la amani.
Mwisho.

Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD