TANGAZO
Mkuu wa jeshi la polisi Tz Ernest Mangu. |
Dhamana inatolewa bure, hakuna malipo yoyote yanayotakiwa
kutolewa ili mtuhumiwa au mshtakiwa akubaliwe dhamana.
Jambo la msingi ni mtuhumiwa kuomba apewe dhamana na
kutimiza taratibu kwa muijibu wa sheria.
Vigezo vya kuzingatia kabla ya mtuhumiwa kabla ya kupewa dhamana ya Polisi.
Vigezo vya kuzingatia kabla ya mtuhumiwa kabla ya kupewa dhamana ya Polisi.
Polisi kujiridhisha kwamba mtuhumiwa atatimiza masharti ya
dhamana atakayopewa, ikiwa kufika siku na saa atakayoamriwa.
Kujua makazi,ndugu na jamaa, ajira na ikibidi hali ya maisha ya
mtuhumiwa na familia yake, kumbukumbu za kihalifu kama zipo.
Umuhimu wa mtuhumiwa kuwa nje kwa dhamana, ili aweze kujiandaa
kukabiliana na tuhuma zinazomkabili kabla ya hajafikishwa mahakamani mfano
kupata msaada wa kisheria
KUKATALIWA DHAMANA YA POLISI
Kifungo cha 67 cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai
kinaeleza kwamba, mtuhumiwa aliye chini ya ulinzi wa Polisi anaweza kukataliwa
maombi yake ya kutaka apewe dhamana
KUFUTWA KWA DHAMANA YA POLISI
Baada ya mtuhumiwa kupewa dhamana ya Polisi na kuwa huru dhamana
hiyo inaweza kufutwa na mkuu wa kituo , chini ya kifungu cha 68 cha sheria ya
mwenendo wa makosa ya jinai. Baadhi ya sababu zinazoweza kusababisha uamuzi
wakufuta dhamana ni:-
(a) Kubainika kwamba mtuhumiwa anapanga mipango ya kutoroka
(b) Kwa makusudi anakiuka au yu karibu kukiuka masharti ya dhamana
(a) Kubainika kwamba mtuhumiwa anapanga mipango ya kutoroka
(b) Kwa makusudi anakiuka au yu karibu kukiuka masharti ya dhamana
ADHABU KWA KUKIUKA MASHARTI YA DHAMANA
Dhamana inayotolewa na Polisi kwa mtuhumiwa anayekabiliwa na
kosa la jinai inapaswa kuheshimiwa. Kifungu cha 69 cha sheria ya mwenendo wa
makosa ya jinai kinatoa adhabu kali kwa mtuhumiwa na mdhamini au wadhamini
wanapokiuka masharti ya dhamana waliopewa.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD