TANGAZO
Christopher Lilai,Liwale.
Halmashauri
ya wilaya ya Liwale,mkoani Lindi imefanikiwa kukusanya mapato ya kiasi cha
shilingi Bilioni 1.2 kutokana na ada mbalimbali zinazotokana na mauzo ya mazao
ya misitu ambayo ni zaidi ya lengo lililowekwa.
Akitoa
taarifa ya utendaji na uwajibikaji wa halmashauri hiyo kwa kipindi
cha mwaka mmoja(julai2014 hadi juni 2015) kwenye kikao
cha baraza la madiwani mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi mtendaji wa
halmashauri hiyo,Gaudence Nyamwihura alibainisha kuwa kiasi hicho
kilikusanywa kutoka kwenye ada za leseni ,mauzo ya mbao,tozo mbalimbali kwa
waharifu na ushuru wa mkaa.
Alitaja
vyanzo vingine ni ada ya usajili na hati za kusafirisha mazao ya misitu,ushuru
wa milango,kabati,vitanda na makochi.
Nyamwihura
alieleza kuwa katika kiasi hicho kilichokusanywa kiasi cha shilingi
Bilioni 1.1 ni za serikali kuu,milioni 52,406,964 ni fedha
zinazotozwa kwa ajili ya upandaji wa miti na kiasi cha shilingi milioni
56,092,363 ni za halmashauri ya Liwale.
Alibainisha
kuwa mafanikio ya ukusanyaji huo umetokana na kufanyika kwa doria za mara kwa
mara ambapo doria zipatazo 38 zimefanyika katika misitu ya hifadhi ya Ngera,
kipelele,Angai na katika barabara ya Liwale hadi Nachingwea na ile ya
Liwale na Nangurukuru.
Alisema
kuwa katika doria hizo watu 6 walikamatwa na kufikishwa mahakama ya wilaya,mbao
zipatazo 4,075 za mininga na mkongo zilikamatwa kwenye misitu ya Ngera
,Kipelele,misumeno ya mnyororo miwili ilikamatwa,misumeno ya mkono 35 pia
ilikamatwa na baiskeli moja ilikamatwa ambapo jumla ya mbao 1,100
ziliuzwa kwa njia ya mnada.
Alibainisha
kuwa kwa kipindi hicho halmashauri hiyo iliwezesha vijiji 13 kushiriki katika
mpango wa usimamizi shirikishi wa misitu .
Alisema
kuwa kati ya vijiji hivyo vilivyowezeshwa, vijiji vya
Mtungunyu,Nahoro,Kiangara, Nangano, Legezamwendo,Mikunya,Ngongowele,Mikuyu na
Ngunja vimewezakuhifadhi misitu yao kama hifadhi ya vijiji ambapo jumla ya
hakta za misitu 85,868.1 zimeifadhiwa na kumilikiwa na vijiji hivyo.
Licha ya
mafanikio hayo Nyamwihura alizitaja changamoto kadhaa inayokabidi idara ya
misitu na kufanya ishindwe kutekaleza majukumu yake ipasavyo ambapo alitaja
changamoto ya usafiri magari na raslimali fedha kwa ajili ya doria.
Alitaja
changamoto zingine kuwa ni ufyekaji wa misitu kwa ajili ya kilimo cha ufuta,
baadhi ya wafanyabiashara wa mbao kuendelea kuvuna mbao katika misitu ya
hifadhi kinyume na sheria na ushiriki mdogo kutoka kwa jamii katika kushiriki
shughuli za usimamizi wa misitu.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD