TANGAZO
Mkutano Mkuu wa Umoja
wa Wanawake Tanzania (UWT) umemalizika muda mfupi uliopita kwenye Ukumbi wa
Emirates mjini Masasi huku wajumbe hao
wakiwarudisha tena madarakani waliokuwa wabunge wa UWT wanawake mkoa wa Mtwara katika kipindi cha Miaka mitano Iliyopita
ambao ni AGNESS ELIAS HOKORORO NA ANASTANSIA J. WAMBURA.
MWENYEKITI wa Muda wa Mkutano Mkuu wa UWT mkoa wa Mtwara akiwa kwenye picha ya pamoja na wagombea walioshinda kwenye uchaguzi uliofanyika hii leo kwenye ukumbi wa Emirates Mjini Masasi.Kushoto kwake ni Mheshimiwa Agness Hokororo na kulia kwake ni Mheshimiwa Anastansia Wambura.Aliowashika mikono ni wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi huo kutoka vyuoni.
MGOMBEA Emma Rashidi Kawawa aliyeshindwa kwenye Uchaguzi wa umoja wa wanawake Tanzania (UWT) kwa kuambulia kura 40.Huyu ni mtoto wa marehemu Mzee Rashidi Mfaume Kawawa.
MSIMAMIZI Mkuu wa Uchaguzi wa umoja wa wanawake Tanzania (UWT) ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego akitangaza matokeo ya uchaguzi huo leo kwenye ukumbi wa Emirates mjini Masasi.
MHESHIMIWA Anastansia J. Wambura akitoa shukrani kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa UWT Mkoa wa Mtwara kwa Kumchagua tena kushika wadhifa huo wa ubunge wa viti maalumu kupitia UWT.
MHESHIMIWA Agness Elias Hokororo akitoa shukrani kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa UWT Mkoa wa Mtwara kwa Kumchagua tena kushika wadhifa huo wa ubunge wa viti maalumu kupitia UWT.
Katika Kuonesha kuwa Umoja Ni Ushindi...Mgombea aliyeshinda ambaye ni Agness Hokororo akimpongeza mgombea mwenzake aliyeshindwa Rukia Swalehe Liumba baada ya kutangazwa kwa matokeo.
MATOKEO YA JUMLA:
WAGOMBEA-09
IDADI YA WAJUMBE-664
KURA HALALI-662
KURA
ZILIZOHARIBIKA-02
1.Anastansia J.
Wambura Kura 438
2.Agness Elias
Hokororo kura 316
3.Rukia Swalehe
Liumba kura 223
4.Daisy Jafari
Ibrahimu Kura 204
5.Emma Rashid Kawawa
kura 40
6.Luckiness Adrian
Amlima Kura 12
7.Dr.Divana Donald
Kaombe Kura 11
8.Asha Salumu Motto
kura 08
9.Thecla Robert Mbuki
Kura 01.
BAADHI ya wagombea walioshinda na walioshindwa wakiwa kwenye picha ya pamoja na mwenyekiti wa muda wa mkutano wa UWT Mama Anna Abdallah.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD