TANGAZO
BAADHI ya Wagombea wanaowania Kuteuliwa na Mkutano Mkuu wa UWT mkoa wa Mtwara kuwa wabunge wa viti maalumu mkoani Humo kutoka kushoto ni Rukia Liumba,Daisy Ibrahimu,Emma Kawawa na Asha Salumu Motto wakiwa ndani ya ukumbi wa mikutano wa Emirates mjini Masasi hii leo.
Mheshimiwa Hawa Ghasia akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa UWT mkoa wa Mtwara hii leo kwenye ukumbi wa Emirates Mjini Masasi.
MKUTANO mkuu maalumu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Mtwara umeanza muda mfupi uliopita huku ukihudhuriwa na wajumbe 664 kati ya wajumbe 675 waliotakiwa kuhudhuria.
Agenda kuu ya mkutano huo ni uchaguzi
wa wabunge wa viti maalumu wanawake mkoa wa Mtwara watakaowawakilisha wenzao kwenye
bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa
mkutano huo mgeni rasmi ambaye ni waziri wan chi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Hawa Ghasia amesema huu ni wakati muafaka kwa
wanawake wa jumuiya hiyo kote nchini kufanya maamuzi magumu kwa kuchagua watu
wenye msimamo na wenye uchungu wa maendeleo katika mikoa yao.
Alisema wanawake wamekuwa na tabia ya
kuoneana aya wakati wa uchaguzi mazingira yanayopelekea kila siku kupatikana
kwa viongozi wabovu na wasio na uchungu na maendeleo huku wakishindwa kabisa
kutekeleza ilani ya CCM.
“Wako baadhi ya wabunge ambao hawana
mchango wowote kwa wananchi wao waliowachagua wamebaki kuwa mizigo viongozi
kama hao kwa sasa ndani ya CCM hawana nafasi”.alisema Ghasia.
Wanaowania Kuchaguliwa na wajumbe hao
ni makada tisa wakiwemo Daisy Jafari Ibrahimu,Asha Salumu Motto,Rukia Swalehe
Liumba,Agness Elias Hokororo,Luckiness Adrian Amlima,Anastansia J.
Wambura,Divana Donald Kaombe,Thecla Rogath Mbiki pamoja na Emma Rashidi Kawawa.
Wajumbe wa Mkutano huo ni kutoka
katika wilaya zote za mkoa wa Mtwara zikiwemo Masasi,Nanyumbu,Tandahimba,Newala,Mtwara
Vijijini, na Mtwara Manispaa.
BAADHI ya wapambe wakifanya kampeni za mwisho kabla ya Uchaguzi huo hii leo Asubuhi wakiwa nje ya ukumbi wa Emirates Mjini Masasi.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD