Loading...
ADVERTISE WITH US ON THIS BLOG.CALL +255 714 789 592/ +255 682 997 767/ +255 752 944 022

MAELFU YA WATU WAMZIKA MFANYAKAZI WA HALMASHAURI YA MJI WA MASASI

TANGAZO
Marehemu Pendo S. Malimilo alizaliwa Machi 19,1978 huko katika kijiji cha Mbati Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.

Alipata elimu ya Msingi katika shule ya msingi Nalasi kati ya mwaka 1986-1992.Mwaka 1993 alijiunga na elimu ya sekondari Tunduru na alifanikiwa kuhitimu mwaka 1996.

Mwaka 1996 -2001 marehemu alipata cheti cha ualimu daraja la III A katima Chuo cha Ualimu Nachingwea Mkoani Lindi.

Mwaka 2002 marehemu Pendo Malimilo aliajiriwa kama mwalimu katika Halmashauri ya wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma na baadae mwaka 2005 alihamia Halmashauri ya wilaya ya Masasi mkoani Mtwara.

Alijiendeleza kimasomo katika chuo cha kumbukumbu ya mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam katika mafunzo ya maendeleo ya jamii na kuhitimu mwaka 2010.

Mwaka 2012 baada ya mgawanyo wa Halmashauri ya wilaya ya Masasi na Halmashauri ya mji wa Masasi Marehemu alihamia Halmashauri ya mji wa Masasi kama mwalimu ambapo baadae alibadilishwa kada na kuwa Ofisa Maendeleo ya Jamii na hii ni baada ya kujiendeleza katika fani hiyo.

Mamia ya wakazi wa mji wa Masasi na wilaya jirani wakiwa wamebeba jeneza la marehemu Pendo S. Malimilo.

Marehemu alikuwa anasumbuliwa na Ugonjwa wa Ini na hatimaye Julai 23,2015 majira ya saa 10:30 jioni alifariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa matibabu.

Marehemu ameacha Mume na Mtoto mmoja wa Kike

 MSAFARA wa magari ukimsindikiza marehemu Pendo katika safari yake ya Mwisho.
Msafara wa magari na pikipiki na waenda kwa miguu wakiwa kwenye shughuli ya kuusindikiza mwili ya marehemu Pendo S. Malimilo.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mtazamo Mpya | Designed By FAHARI YA TANZANIA
Back To Top