TANGAZO
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Masasi Juliana Sowani. |
MKUTANO mkuu maalumu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara umeanza hii leo muda mfupi uliopita huku ukihudhuriwa na wajumbe 1054 kati ya wajumbe 1126 waliotakiwa kuhudhuria.
Agenda kuu ya mkutano huo ni uchaguzi
wa madiwani wa viti maalumu wanawake kutoka wilaya ya Masasi watakaowawakilisha
wenzao kwenye mabaraza ya madiwani katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
KATIBU wa UWT Wilaya ya Masasi Bi. Joyce Mkaugara akizungumza wakati wa mkutano huo unaoendelea kwenye ukumbi wa Emirates Mjini Masasi. |
Madiwani hao wa viti maalumu wanawake
ni wale watakaowakilisha kwenye baraza la madiwani la Halmashauri ya wilaya ya
Masasi pamoja na lile la Halmashauri ya mji wa Masasi.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa
mkutano huo Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Masasi Juliana Sowani alisema huu ni
wakati muafaka kwa wanawake wa jumuiya hiyo kote nchini kufanya maamuzi magumu
kwa kuchagua watu wenye msimamo na wenye uchungu wa maendeleo katika kata zao.
WAJUMBE wa Mkutano Mkuu wa UWT wilaya ya Masasi wakiwa kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Emirates Mjini Masasi.
Alisema wanawake wamekuwa na tabia ya
kuoneana aya wakati wa uchaguzi mazingira yanayopelekea kila siku kupatikana
kwa viongozi wabovu na wasio na uchungu na maendeleo huku wakishindwa kabisa
kutekeleza ilani ya CCM.
Umoja wa wanawake Tanzania (UWT)
wilaya ya Masasi una jumla ya wanachama wapatao 17,000 huku wanawake
waliojitokeza kwa mwaka huu 2015 kuwania kuchaguliwa kwenye nafasi hizo ni 56
ambapo idadi halisi ya wanaotakiwa ni 16.
Wajumbe wa Mkutano huo ni kutoka
katika tarafa sita za Chikundi,Lisekese,Chigugu,Masasi,Mchauru, na Chiungutwa.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD