TANGAZO
MMOJA wa majeruhi ambaye alikimbizwa katika Hospitali ya Mkomaindo Mjini Masasi Baada ya kupata mshtuko wa mlipuko huo wa umeme kwenye ukumbi huo wa Emirates.
Ni mmoja wa wanawake wa mkutano mkuu wa UWT wilaya ya Masasi akipata huduma ya kwanza kutoka kwa wauguzi wa Hospitali ya Mkomaindo Mjini Masasi baada ya kutokea tafrani kwenye ukumbi wa Emirates ulionusurika kuwaka Moto.
" Baadhi ya wajumbe wamepata majeraha madogo
madogo huku mmoja kati yao akikimbizwa katika Hospitali ya Mkomaindo kwa
matibabu zaidi,wajumbe waliopata majeraha ni pamoja na Rukia Matogoro,Hilda
wadi,Herieth Evance,Zuena Mtendechi,Fatu Issa,Mary Mlaponi na Mtoto Nasra Sadam
(08)."
MUUGUZI akiwa kazini wakati anatoa huduma kwa mmoja wa walioumia kwenye sekeseke la ukumbi wa Emirates kuwaka moto.
WAJUMBE wa Mkutano Mkuu wa UWT wilaya ya Masasi wakiwa nje ya ukumbi wa mikutano wa Emirates wakishindwa kuamini kilichotokea na wao kunusurika huku wengine wakidai kuwa hawawezi kurudia kuingia tena ndani ya ukumbi huo.
Wajumbe wakiwa nje ya ukumbi baada ya kutoka ndani
BAADHI ya wanawake wa UWT wakisukumana Mlangoni huku kila mmoja akitaka kujiokoa
Wajumbe wakiwa nje ya Ukumbi
"Akizungumza mmoja wa mafundi wa shirika la Umeme
Tanzania TANESCO wilaya ya Masasi waliofika eneo la tukio kwa ajili ya kufanya
marekebisho ya mfumo wa umeme kwenye jengo hilo alisema tatizo lilikuwa kwenye
nyanya za umeme zinazoingia kwenye jengo hilo kushindwa kuhimili kufanya kazi
kwa muda mrefu kutokana na vifaa vinavyotumika kwenye jengo hilo kuwa vingi"
MMOJA wa wajumbe waliopata majeraha ya mguuni
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD