TANGAZO
Na Christopher Lilai,Lindi.
Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM,Nape Nnauye ni miongoni mwa wanachama
wapatao 33 wa Chama cha mapinduzi (CCM) mkoani Lindi,waliojitokeza kuchukua
fomu za kuomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea ubunge katika majimbo manane
yaliyopo mkoani hapa.
Nape anawania nafasi hiyo kwenye jimbo la
Mtama,sambamba na kada mwingine wa chama hicho, Selemani Mathew mchezaji wa
zamani wa Yanga, ili wawe warithi wa Waziri wa mambo ya nje na ushiriano wa
kimataifa.Bernad Membe ambaye alitangaza kutogombea tena ubunge jimboni humo.
Kwa mujibu wa Katibu Chama cha mapinduzi (CCM) mkoani
Lindi,Adelina Gec, wakati anazungumza na waandishi wa Habari alisema idadi
ya wanachama hao waliojitokeza kuchukuwa fomu ni kubwa ukilinganisha na miaka
ya nyuma.
Aliwataja wanachama wengine waliojitokeza na majimbo yao
kwenye mabano kuwa ni,Fadhili Abdallah Magoma na Francis Kumba Ndulane (Kilwa
kaskazini), Kassimu Majaliwa na Bakari Nampenya (Ruangwa),Selemani Mathew
Luhongo,Rukia Abdallah Mandindi,Isumaili Selemani Mbuni, Nape Moses Nnauye, Markis
Marki na Jeneth Mayanje (Mtama).
Wengine ni,Zainabu Kawawa,Haji Munde,Mshamu Ally (Liwale),Said
Ally Timami,Hafidhi Bakari,Asnen Ghullam Dewji,Sowami Omari Kisongo (Kilwa kusini).
Kwa Upande wa jimbo la Lindi Mjini ni Abubakari Said Maguo,Masoud
Ally Mikorogo,Abukari Kadhi Abubakari,Hassani Mohamedi Jarufu,Tika Hamisi
Omari,Hassani Selemani Kaunje,Mohamed Kateva,Masoud Mikorogo, Adinani
Livamba,Mohamed Uthali na Daudi Msungu.
Jimbo la Mchinga waliochukua fomu ni,mbunge anayetetea nafasi hiyo
Said Mtanda,Yusuf Amani, Adamu Kulagwa, Dk,Alawi Mikidadi,Mehdoody
Othman,Fatuma Abdallah Mikidadi, Ridhiki Lulida na Mikidadi Kumtungwa.
Nako jimbo la Nachingwea
waliojitokeza ni, Fadhili Ally Liwaka, Issa Mohamedi Mkalinga,Baneto
Ng’itu,Ally Abdallah Namnyundu. Mathias Chikawe, Hasani Masala na Mwenyekiti wa
chama hicho wa wilaya ya Nachingwea,Albert Mnali na Steven Nyoni,
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD