TANGAZO
Na Fatuma Maumba,Mtwara.
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda, amesema viongozi wote ambao wamebahatika
kuchaguliwa katika uchaguzi wa Serikali za mitaa ambao ulifanyika mwishoni mwa
mwaka jana, watapata fursa ya kupata mafunzo ili waweze kusimamia shughuli
mbalimbali za maendeleo, ikiwemo huduma za jamii pamoja na shughuli
za ulinzi na usalama katika maeneo yao.
Pinda aliyasema hayo jana wakati akiwahutubia wananchi wa Mtwara kwenye
uwanja wa Mashujaa wakati akifunga maadhimisho ya sherehe ya serikali za mitaa
ambayo kitaifa yamefanyika mkoani humo.
Alisema viongozi watakaopatiwa mafunzo
hayo ni wale ambao wameingia kwa mara ya
kwanza katika uongozi ili waweze kutekeleza majukumu yao kiufanisi zaidi.
Aidha waziri Pinda, amevitaka vyama
vya siasa nchini viwasaidie wananchi wa Mtwara na kuwaandaa vizuri waanze
kuwaelekeza zaidi namna watakavyotumia fursa hiyo badala ya kuwachonganisha
jamii na vyombo vinavyosimamia sera.
Hata hivyo waziri mkuu huyo alisema mfuko
wa maendeleo ya jamii TASAF awamu ya tatu umekuja tofauti kidogo, kwani awamu
hii umekuja kuwezesha kaya maskini ili kuweza kuongeza kipato na fursa za
kiuchumi huku akizitaka Halmashauri zote nchini kufanyakazi kwa
ukaribu na Mfuko huo ili kaya maskini za kweli ndizo ziwe walengwa wakubwa.
Maadhimisho ya sherehe ya wiki ya
Serikali ya Mitaa ambayo yamefanyika Kitaifa mkoani Mtwara
yameitimishwa jana Mkoani humo ambayo yalifunguliwa juni 26 mwaka huu na Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI,Hawa
Ghasia.
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo kwa
mwaka huu ni Mwananchi pigia kura katiba
pendekezwa na chagua viongozi bora kwa maendeleo endelevu baada ya mwaka 2015.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD