TANGAZO
Jumla ya makada 45 wa chama cha
mapinduzi mkoa wa Mtwara wamerejesha fomu huku mgombea mmoja Selemani Libuburu
aliyechukua fomu kuwania ubunge jimbo la Mtwara Vijijini Julai 18,2015
akishindwa kurejesha fomu kutokana na kushindwa kutimiza
vigezo na kanuni za CCM zinavyoelekeza.
Kwa mujibu wa katibu wa CCM mkoa wa
Mtwara Shaibu Akwilombe ratiba nzima ya mchakato wa chama hicho katika kuwapata
wagombea wake katika majimbo yote 10 mkoani humo inaonesha kuwa kampeni za
ndani ya chama zinatarajia kuanza Julai 26 mwaka huu na kwamba watia nia wote
watapita kila kata kuomba kura kwa wanachama.
KATIBU wa CCM mkoa wa Mtwara Shaibu Akwilombe
Katika jimbo la Lulindi waliorejesha
fomu ni Jerome Bwanausi,Enock Richard na Thomas
Sowani wakati kwa jimbo la Ndanda ni Mariam Kasembe,Reinald Mrope na Cisilu
Mwambe huku jimbo la Masasi ni Geoffrey
Mwambe, Mike Mande, Rashid
Chuachua,Margreth Mtaki, Joseph Nkata,Joshua Nnonjela,Edwin Eckon pamoja na
Regnald Kombania.
Mariam Kasembe amerejesha Fomu Katika Jimbo la Ndanda
Bwana Geoffrey Katali Mwambe Mtia nia Jimbo la Masasi.
Rashid Chuachua Mtia nia ya Ubunge Jimbo la Masasi
Jerome Bwanausi Mgombea Ubunge Jimbo la Lulindi
Wanachama wa CCM
waliorejesha fomu jimbo la Mtwara mjini ni pamoja na Hussein Kasugulu,Said
Swala,Mussa Chimae,Hasnen Murji na Salumu Nahodha,huku jimbo la Nanyamba likiwa
na makada wawili waliorejesha fomu ambao ni Swalehe Livanga na Abdallah
Chikota.
Mussa Chimae Mgombea Ubunge Jimbo la Mtwara Mjini
Asnen Murji Mgombea Ubunge Jimbo la Mtwara Mjini aliyeshika Boksi.
Abdallah Chikota Jimbo la Nanyamba
Aidha kwa upande
wa jimbo la Mtwara vijijini aliyerejesha fomu ni mwana CCM mmoja pekee Hawa
Ghasia kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kukosa upinzani ndani ya chama chake.
Hawa Ghasia Mgombea Pekee wa nafasi ya Ubunge Jimbo la Mtwara Vijijini
Jimbo la
Tandahimba limewakutanisha makada watano wa chama hicho wakipigana vikumbo
kuwania nafasi hiyo ya kuwatumikia wananchi wanaowania ubunge jimboni humo ni
pamoja na Rajabu Mmunda, Justin Nandonde, Dkt.Ally Mandali, Likumbo Shaibu na
Dkt.Bahati Issa.
Ushindani mkubwa
upo kwenye jimbo la Newala mjini ambako mwanasiasa mkongwe nchini kapteni
mstaafu George Huruma Mkuchika amejitokeza kwa mara nyingine tena kuomba ridhaa
kutoka kwa wana CCM wa jimbo hilo huku akipata upinzani mkali kutoka kwa Rajabu
Kazibure na Kwame Andrew Daftari.
Kapteni Mstaafu George Huruma Mkuchika Jimbo la Newala Mjini.
Kwa jimbo jipya la Newala Vijijini makada wanane
wamejitokeza ikiwa ni pamoja na Abasi Mnyalumkuwaje,Haji Mnasi,Fakihi
Mshamu,Fatuma Machinga,Rashidi Taka,Haroun Maarifa,Yahya Nawanda pamoja na
Rashidi Akbal.
Haji Mnasi Jimbo la Newala Vijijini
Huko Nanyumbu
nako vigogo kadhaa wa serikali wamejitokeza kuchukua na kurejesha fomu
wakichuana na mbunge aliyemaliza muda wake Dastan Makapa,wengine ni pamoja na
William Dua,Wema Issa,Yahaya Mhata,Andrew Napacho,Harid Uledi na Majaribu
Lupeto.
Dastan Mkapa Mgombea Jimbo la Nanyumbu
Aidha wanachama
wa CCM waliogombea nafasi za uongozi kupitia umoja wa vijana wa CCM (UVCCM)
mkoa wa Mtwara ni Diya Mwaya,Mwajuma Abasi na Mshihiri Mwaneno wakati kwa
upande wa nafasi ya umoja wa jumuiya ya wazazi waliojitokeza ni Didie Mlaka,Hawa Salumu Chikuyu na Zuhura Mikidadi.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD