TANGAZO
Na Clarence Chilumba,Masasi.
Mhariri mtendaji wa gazeti la The African linalochapishwa na kampuni ya
New Habari (2006) Ltd,Mike Mande amejitosa kwenye Kinyang’anyiro cha Ubunge
Jimbo la Masasi kupitia Chama cha Mapinduzi.
Mande alisema lengo la kuomba ridhaa hiyo ya kuchaguliwa na wana CCM ni
kuleta maendeleo jimboni humo huku akisisitiza umoja na upendo miongoni mwa
watia nia wote wanaoomba ridhaa ya kuchaguliwa na wana CCM hao wa wilaya ya
Masasi.
Wengine waliochukua fomu ni pamoja na Geofrey Mwambe,Regnald
Kombania,Cleveland Nkata,Margreth Mtaki,Edwin Eckon,Joshua Nnonjela na Rashid
Chuachua.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD