Loading...
ADVERTISE WITH US ON THIS BLOG.CALL +255 714 789 592/ +255 682 997 767/ +255 752 944 022

MAKADA 14 WA CCM WILAYA YA MASASI WALIOTIA NIA YA UBUNGE WAREJESHA FOMU ZAO

TANGAZO
Bwana Geoffrey Katali Mwambe Mmoja wa wagombea hao.
 Na Clarence Chilumba,Masasi.
Tukiwa tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu wa Madiwani,Wabunge na Rais Oktoba mwaka huu tayari jumla ya makada 14 wa chama cha mapinduzi wilaya ya Masasi wamerejesha fomu huku ushindani mkubwa ukiwa ni kwenye jimbo la Masasi ambalo hadi sasa waliorejesha fomu ni wagombea saba.
Aidha ushindani unaonekana jimbo la Masasi kutokana na aina ya wagombea wake waliotangaza nia na kurejesha fomu wakiwa na sifa lukuki ambazo zinaweza kuwapa ugumu wajumbe wa chama cha mapinduzi watakaoketi kupendekeza jina moja la mgombea wa chama hicho.
Kitu kingine kinachochangia ugumu wa kumpata mgombea wa chama hicho atakayesimama kugombea kiti hicho cha ubunge jimbo la Masasi ni kutokana na wagombea hao kuwa wageni kwenye nafasi hiyo kwani mbunge wa sasa wa jimbo hilo mariamu Kasembe ameamua kugombea jimbo la Ndanda.
MHESHIMIWA Mariam Kasembe ambaye anamaliza nafasi yake ya ubunge kwa jimbo la Masasi ambapo kwa mwaka huu ametia nia ya kugombea ubunge kwenye jimbo jipya la Ndanda.
Kada mbalimbali zimejitokeza kushiriki kwenye uchaguzi huo lakini cha kufurahisha zaidi kuwa miongoni mwa watia nia hao ni  mwanahabari ambaye ni mhariri wa gazeti la Mtanzania Mike Mande Matwe ambaye nae anaomba ridhaa ya kuchaguliwa na chama cha Mapinduzi wilaya ya Masasi aweze kupeperusha bendera ya chama hicho.
Bwana Geoffrey Katali Mwambe ni Mmoja ya waliotia nia ya ubunge jimbo la Masasi anayeomba Ridhaa ya kuchaguliwa na chama cha Mapinduzi ili aweze kupeperusha bendera ya chama hicho. Kwa sasa ni Mkurugenzi wa biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye amewataka wana CCM wenzake pamoja na wajumbe wa Halmashauri kuu ya Chama hicho jimbo la Masasi  watakaoketi kuchagua jina moja la mgombea wa chama hicho kutenda haki na  maamuzi sahihi katika kumpata mgombea wa nafasi ya ubunge.






DKT. Margreth Mtaki ambaye nae ni mmoja wa watia nia wa nafasi ya ubunge jimbo la Masasi anayeomba ridhaa ya kuchaguliwa na wanachama wa CCM aweze kupeperusha bendera ya chama hicho.
Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara ina majimbo matatu ya Ndanda,Lulindi na Masasi ambapo hadi sasa jumla ya watia nia 14 wamechukua fomu na kuzirejesha jana kwenye ofisi za chama cha mapinduzi wilaya ya Masasi huku ushindani mkubwa ukiwa kwenye jimbo la Masasi ambalo lina jumla ya watia nia saba akiwemo mhariri wa gazeti la Mtanzania Mike Mande.
Bwana Rashid Mohamedi Chuachua nae ametia nia ya kuomba kuchaguliwa na chama cha Mapinduzi wilaya ya Masasi ili nae basi aweze kupeperusha bendera ya chama hicho kwa jimbo la Masasi.
Wengine waliochukua Fomu na Kurudisha jana ni pamoja na Jerome Bwanausi,Enock Richard na Thomas Sowani (Lulindi), Mariam Kasembe,Reinald Mrope na Cisilu Mwambe (Ndanda), Geoffrey  Mwambe, Rashid  Chuachua,Margreth  Mtaka, Joseph  Nkata,Joshua Nnonjela,Edwin Eckon pamoja na Regnald Kombania (Masasi).
 MBUNGE wa sasa wa Jimbo la Lulindi Jerome Bwanausi ambaye nae ametia nia ya kutetea kiti chake kwa awamu ya pili akionesha fedha shilingi 100,000/=  alizochangiwa na wanachama wa chama cha mapinduzi wa kata ya Mbuyuni ili aweze kuchukua fomu ya ubunge kutokana na kukubali uwezo wake katika utendaji wa kazi zake jimboni humo.

BAADHI ya Makada wa chama cha Mapinduzi Wilaya ya Masasi waliotia nia ya kuomba Ridhaa ya Kuchaguliwa na wanachama wa chama hicho wakiwa kwenye ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Masasi jana,walipokuwa wakipewa maelekezo ya namna watakavyoshiriki kwenye zoezi zima la kampeni za ndani ya chama zinazotarajiwa kuanza Julai 25,2015.


Na Hapa Nimekuwekea Moja ya Maneno ya Msingi aliyoongea ya  Bwana Geoffrey Katali  Mwambe mmoja wa watia nia wa nafasi ya ubunge jimbo la Masasi  wakati anahojiwa hii leo asubuhi  na kituo cha Redio Fadhila kilichopo eneo la Migongo Halmashauri ya Mji wa Masasi.

“Jimbo la Masasi limekuwa kama kichwa cha mwendawazimu…nadhani wana Masasi kwa hapa tulipofikia tuseme inatosha wakati wa mabadiliko makubwa ya uongozi ni sasa,tunahitaji mwakilishi anayeumwa na umasikini wetu,mwenye muono wa mbali na atakayepigania maendeleo ya wananchi wote wa Masasi hivyo rai yangu kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya ni kuepuka kurudia makosa”.

Na Kuongeza Kuwa...........................
“Nimefanya mambo mengi sana ndani ya nchi hii nikiwa pale Benki kuu kama mchumi mwandamizi na sasa kwenye wizara ya Afrika Mashariki nikiwa mkurugenzi…si rahisi kuzungumza mambo yote lakini ukweli ni kwamba wana CCM jimbo la Masasi  wanapaswa kuwapima wagombea wa kiti cha ubunge kwa vigezo na nadhani kwa sasa Geoffrey Katali Mwambe anafaa kuwa mbunge wa jimbo la Masasi”.




TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mtazamo Mpya | Designed By FAHARI YA TANZANIA
Back To Top