TANGAZO
BAADHI ya washiriki wa Mafunzo ya ushirikiano wa Uboreshaji wa serikali za mitaa kati ya Tanzania na Osaka nchini Japani kutoka kwenye Halmashauri zote za Mkoa wa Mtwara wakifuatilia kwa Karibu Mada kutoka kwa mwezeshaji wakati wa mafunzo hayo kwenye ukumbi wa NAF Apartment Manispaa ya Mtwara hii leo.
Kutoka Kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mtwara Julius Kaondo,Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Nanyumbu Ally Kasinge,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyamba Oscar Ng'itu wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali wakati wa mafunzo hayo.
Washiriki wa Mafunzo ya siku nne ya ushirikiano wa uboreshaji wa serikali za mitaa kati ya Tanzania na Osaka nchini Japan yanayoendelea kwenye ukumbi wa NAF Apartment Manispaa ya Mtwara Mikindani.
KATIBU Tawala wa Mkoa wa Mtwara Alfred Luanda akizungumza wakati wa Ufunguzi wa mafunzo ya ushirikiano wa Uboreshaji wa Serikali za Mitaa kati ya Tanzania na Mji wa Osaka nchini Japan hii leo.
MKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Bwana Julius Kaondo akizungumza wakati akitoa shukrani kwa Mgeni Rasmi ambaye ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwata Alfred Luanda.
Baadhi ya maofisa Habari wakiwa Kwenye Mafunzo hayo wa kwanza kulia ni Evarist Masuha Ofisa Habari Mkoa wa Mtwara na anayefuatia ni Bi.Joyna Nzali Ofisa Habari Halmashauri ya wilaya ya Masasi.
Kulia ni Ofisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Mji wa Masasi Zuena Ungele na Ofisa Rasilimali watu wa Halmashauri ya Mji wa Masasi Prisca Manjonda wakiwa kwenye mkutano Unaoendelea mjini Mtwara.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD