Loading...
ADVERTISE WITH US ON THIS BLOG.CALL +255 714 789 592/ +255 682 997 767/ +255 752 944 022

IFAHAMU HISTORIA YA MGOMBEA WA URAIS KWA TIKETI YA CCM DKT.JOHN POMBE MAGUFULI

TANGAZO
 Mgombea wa urais wa chama cha CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2015 Daktari John Pombe Joseph Magufuli ni mbunge wa jimbo la Chato lililoko mkoa wa Geita na ni waziri wa ujenzi wa Tanzania.
Alizaliwa tarehe 29 Oktoba 1959 wilayani Chato Mkoani Kagera.
Kielimu, daktari Magufuli ana Stashahada ya elimu ya sayansi akibobea kwenye masomo ya Kemia, Hisabati.
Mgombea huyo wa urais ana shahada ya umahiri wa Sayansi na shahada ya uzamivu ya kemia.
Aidha daktari Magufuli amewahi kufundisha katika shule ya sekondari Sengerema miaka ya themanini kisha akajiunga na mafunzo ya JKT.
wajumbe wa mkutano mkuu wa Chama cha Mapinduzi wakishangilia baada ya mwenyekiti wa chama hicho kutangaza kuwa Dkt.John Magufuli ndiye mgombea wa urais kupitia CCM.
Alipohitimu, daktari Magufuli na aliaanza kufanya kazi katika kiwanda cha ‘Nyanza Cooperative Union akiwa Mkemia kabla ya kuondoka hapo na kuwania ubunge.
Magufuli alianza mbio za ubunge mwaka 1995 katika jimbo la Chato na kushinda kisha akateuliwa na Rais Benjamin Mkapa kuwa naibu waziri wa Miundombinu.
Katika uchaguzi wa Mwaka wa 2000 pia aligombea ubunge na kushinda na Rais Mkapa akamteua kuwa Waziri wa miundombinu.
Alianza siasa mwaka 1995.

Dkt.John Pombe Magufuli akizungumza baada ya kutangazwa kuwa ndiye atakayepeperusha Bendera ya CCM oktoba mwaka huu kwenye uchaguzi mkuu.
Katika uchaguzi wa mwaka 2005 daktari Magufuli aligombea ubunge kwa mara ya tatu na kupita bila kupingwa.
Rais Kikwete alimteua kuongoza wizara ya Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi na baadaye akamhamishia hadi wizara ya Mifugo na uvuvi.
Mwaka 2010 alichaguliwa kuwa mbunge kwa mara ya nne na Rais Kikwete alimrudisha katika Wizara ya Miundombinu na ujenzi.
Siku aliyochukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuchaguliwa na wana CCM
Daktari Magufuli anachukuliwa kuwa ni mwanasiasa mwenye msimamo thabiti, mchapa kazi na asiye yumbishwa au hata kufuata upepo wa kisaisa.
Anatambulika kuwa Mchapa kazi
Watanzaniania wanamkumbuka kwa usimamizi na ujenzi wa barabara na majengo thabiti.
Anakumbukwa kwa kuchukua hatua za kutoa amri za kubomolewa kwa majengo ya kifahari ambayo alihisi yalikiuka sheria za ujenzi.
Na alipokuwa waziri wa Maendeleo ya Mifugo, Bwana John Magufuli alikwenda hadi bandari ya Dar-es-Salaam na kuizuia meli ya wachina iliyokuwa inashukiwa kufanya uvuvi haramu katika sehemu ya bahari ya Tanzania.


 Ulinzi nao Uliimarishwa nje ya ukumbi wa mikutano wa CCM mkoani Dodoma.
 Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wakiwa katika pilikapilika mjini Dodoma.
 Dkt.Magufuli enzi za ujana wake




TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mtazamo Mpya | Designed By FAHARI YA TANZANIA
Back To Top