TANGAZO
Christopher
Lilai,Ruangwa.
Halmashauri
ya wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi inatarajia kuingiza kiasi cha shilingi
bilioni 2 kila mwaka ikiwa ni fedha ya kodi itokanayo na asilimia
0.3 ya mapato ghafi ya madini ya Kinywe yaliyogunduliwa wilayani humo.
Hayo
yalibainishwa mwishoni mwa wiki na Meneja mahusiano wa kampuni ya
Uranex Tanzania Limited ambayo ndio inayotarajia kuanza shughuli za uchimbaji
wa madini hayo wilayani hapa mwanzoni mwa mwaka ujao,Leah
Mafwenga katika semina ya kuwajengea uelewa madiwani wa Halmashauri ya wilaya
ya Ruangwa.
Alisema
utafiti wa awali unaonesha kuwa katika eneo hilo lenye ukubwa wa kilometa za
mraba 198.57 kuna tani milioni 156 za mashapo ya Kinywe na kuwa ni
mgodi mkubwa kuliko migodi yote ya madini hayo katika Bara la Afrika hivyo
kufanya nchi ya Tanzania kuwa ni mzalishaji mkubwa wa madini hayo.
Alisema dalili
za uwepo wa madini ya Kinywe katika eneo la mradi zilianza kuonekana mwishoni
mwa mwaka 2012 na kuwa hii ilifuatiwa na uchongaji wa kina wa miamba
na kuwa kwa sasa kampuni imebaini maeneo kadhaa yenye
mashapo ya madini ya Kinywe.
“Kufuatia
kubaini uwepo wa madini hayo katika maeneo mbalimbali ya wilaya hii tunakusudia
kuchagua eneo lenye daraja la juu la mashapo kwa ajili
ya kufanya vipimo vya uchenjuaji na kuandaa upembuzi yakinifu”alisema
Leah.
Aliyataja
maeneo ambayo yameonekana kuwa na madini hayo kuwa ni vijiji
vya Chunyu,Mihewe,Matambarale,Chikwale,Namikulo,Chiundu,na Nangulugai.
Alisema
kwa sasa kampuni hiyo inaendelea kutoa elimu ya sheria ya uwekezaji
wa madini kwa umma ili kuepuka migogoro inayoweza kujitokeza katika hatua
mbalimbali kabla ya kuanza kwa mgodi wa uchimbaji wa madini ya kinywe (bunyu)
hapo mwakani.
Leah
alisema kuwa kampuni pia itatoa mafunzo ya namna ya utunzaji na matumizi bora
ya fedha kwa kaya zote zitakazolipwa fidia kabla ya fidia hizo kulipwa
Akiongea
katika semina hiyo mkurugenzi wa kampuni ya MTL Consulting ambao ndio washauri
wa mradi huu, Johnbosco Tindyebwa alisema kuwa
mradi huo utakuwa ni uwekezaji wa kwanza mkubwa
kufanyika mkoani Lindi na ambao utaweza kutoa ajira za moja kwa
moja kwa watanzania wapatao 400 pindi ukikamilika.
“Kwa hapa
nchini mradi huu ndio utakuwa mkubwa sana ambao utatoa ajira kwa wananchi wetu
wa hapa”alisema Tindyebwa.
Wilaya ya
Ruangwa ni miongoni mwa maeneo machache nchini Tanzania ambayo yamebarikiwa
kuwa na utajiri mkubwa wa madini mbalimbali, ambapo
siku za hivi karibuni kuliibuka mgogoro baina ya mwekezaji wa
madini kampuni ya PACCO GERMS na wanakijiji katika kijiji cha
Mtondo wilayani humu kwa kile kinachosadikiwa kuwa wananchi hao
kukosa elimu juu ya mgodi huo wa dhahabu.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD