TANGAZO
Christopher
Lilai,Lindi.
Chama cha
mapinduzi kimeaswa kudhibiti ugawaji holela wa kadi za chama hicho unaofanywa
na baadhi ya wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi kwa
lengo la kuwabeba.
Hayo
yalisemwa na Kamanda wa vijana wa chama
hicho wilayani Lindi,Seleman Mathew mwishoni mwa wiki wakati anazungumza na
wandishi wa habari kwenye ukumbi wa soko la kijiji cha Mtama mkoani Lindi.
Alisema
endapo vitendo hivyo vinavyofanywa na baadhi ya wanachama wa chama hicho havitadhitiwa mapema itachangia kuwapata
wagombea wasio na uwezo wa kupeperusha
vyema bandera ya chama hicho kwenye uchaguzi ujao.
Alisema
kuwa hivi sasa kuna mlolongo wa kadi ambazo zinatolewa na watu wasiohusika na
utoaji wa kadi ambapo zinapelekwa kwa makatibu wa matawi ambao wanalazimishwa
kugawa kadi hizo kwa wanachama ambao
watampigia kura mgombea wanaemkusudia.
“Tuna
ushahidi wa kutosha kwa sababu kadi hizo tumezihakiki namba na
mbaya zaidi kadi zingine zinatoka maeneo
ya mbali na kusambazwa kwa masharti ya
kumpigia kura mtu Fulani”.alisema Mathew.
Alisema
kuwa wapo wanachama wapatao mia nane ambao wanahitaji kadi lakini hawajapatiwa
hadi hvi sasa kwa kuwa wanadhaniwa kuwa hawana mapenzi na mmoja ya anayedaiwa
kuwa mgombea wa ubunge wa jimbo hilo.
Aidha amewaasa
wanaotia nia ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kutofanya vitendo ambavyo
vinakidhalilisha chama hicho mbele ya jamii.
Alisema
vitendo vya kuingiza kadi kiholela vinafanywa na viongozi wa juu za chama hicho
wenye lengo la kuwabeba baaadhi ya wagombea wanaowataka.
Alimtaka
Katibu wa chama wa wilaya hiyo kuzitoa kadi kwa kufuata taratibu na
sheria kwani zitaleta mpasuko mkubwa ndani ya chama ambao haujawahi
kutokea kwenye jimbo hilo la Mtama.
Alibainisha
kuwa kadi zinatolewa na zinatakiwa kutolewa na makatibu wa matawi na si
vinginevyo kitendo cha wasiohusika kugawa kadi ni kupora kazi ya watendaji hao
wa chama na ukiukwaji wa taratibu za chama.
Aidha
Kamanda huyo aliutaka uongozi wa juu wa chama kutoa haki kwa wagombea wote
katika kufanya mikutano kwani kuna baadhi ya viongozi wa wilaya wanaandaa
ratiba ya kumruhusu mgombea kufanya kampni tena kabla ya wakati.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD