TANGAZO
Na
Clarence Chilumba,Masasi.
HALMASHAURI
ya wilaya ya Masasi mkoani Mtwara imezindua rasmi bodi ya huduma za Afya za Halmashauri lengo
likiwa ni kugatua madaraka kutoka serikali kuu hadi kwa wananachi ambao ndio
waathirika wakubwa wa masuala ya afya ikiwemo vifo vya watoto pamoja na
akinamama wakati wa kujifungua.
Akizungumza
jana wakati wa uzinduzi huo mkuu wa
wilaya ya Masasi Bernald Nduta alisema changamoto kubwa inayoikabili sekta ya
afya nchini ni ukosefu wa dawa na vifaa tiba na kwamba ni vyema sasa serikali
kupitia wizara ya afya na ustawi wa jamii ikatenga fedha za kutosha ili kuweza
kukabiliana na changamoto hizo kupitia bodi hiyo ya afya wilayani humo.
Uzinduzi
wa bodi hiyo ulifanyika jana kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo na kuhudhuriwa
na wakuu wa idara na vitengo,wajumbe wote wa bodi hiyo wakiwemo wa kuchaguliwa (wanaopiga
kura),wawakilishi wa watumiaji huduma za afya kutoka kwenye jamii, makundi
yanayotoa huduma,mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii anayewakilisha
madiwani pamoja na watendaji wa halmashauri hiyo akiwemo mganga mkuu na ofisa
mipango.
Alisema watumishi
wa afya pia wanapaswa kufanya kazi kwa kufuata maadili na kanuni za utumishi wa
umma huku akionya kuwa mtumishi wa idara ya afya atakayebainika kuenenda
kinyume na utaratibu atachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na
kumsimamisha kazi.
Alisema
kwa sasa watumishi wa idara ya afya nchini wamekosa uzalendo mazingira
yanayopelekea kuwapo kwa malalamiko mengi kwenye Hospitali,vituo vya afya na
zahanati za serikali ambapo aliiasa bodi hiyo kufuatilia mara kwa mara utendaji
kazi wa watumishi wa idaara hiyo mara kwa mara.
Kwa
mujibu wa mkuu huyo wa wilaya ya Masasi alitoa agizo kwa ofisi ya mkurugenzi wa
Halmashauri ya wilaya ya Masasi Beatrice Dominick kuhakikisha kuwa wanaandaa
mafunzo haraka iwezekanavyo kwa ajili ya wajumbe wa bodi hiyo ili waweze
kufanya kazi wakijua majukumu yao pamoja na mipaka yao kwa lengo la kuepusha
migongano isiyo ya lazima.
Kwa
upande wake mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Masasi Dkt.Jerry Kanga
alisema uundaji wa bodi za huduma za afya za halmashauri na kamati za vituo ni
utekelezaji wa mabadiliko katika sekta ya afya na serikali za mitaa na kwamba
uhalali wa kuwepo kwa bodi hiyo unatokana na sheria ya serikali za mitaa
(mamlaka za wilaya) sura namba 287.
Alisema moja
ya jukumu kubwa la bodi hiyo ni kuhakikisha jamii inapata huduma bora za afya
inazozimudu,inazozimudu pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa rasilimali na
mgawanyo wake kwa kuzingatia mahitaji katika ngazi zote za huduma na matumizi
bora.
Kwa
mujibu wa Dkt.Kanga alisema pia bodi inawajibu wa kufanya kazi kwa karibu na
Halmashauri ya wilaya pamoja na jamii kwa ujumla ambapo pia inapaswa kupokea
taarifa na kupitia taarifa za utekelezaji wa mipango ya afya ya halmashauri
toka kwa timu ya uendeshaji wa huduma za afya za halmashauri.
Mwisho.
WAJUMBE wa Bodi ya Huduma za Afya za Halmashauri ya wilaya ya Masasi wakifuatilia hotuba ya mkuu wa wilaya ya Masasi Bernald Nduta jana wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD