Loading...
ADVERTISE WITH US ON THIS BLOG.CALL +255 714 789 592/ +255 682 997 767/ +255 752 944 022

BARAZA LA MADIWANI LA HALMASHAURI YA MJI WA MASASI LAVUNJWA RASMI

TANGAZO
 MWENYEKITI wa Halmashauri ya mji wa Masasi ambaye pia ni Diwani wa kata ya Nyasa Mh:Andrew Peter Mtumusha akiongea wakati wa kuvunja Baraza hilo rasmi hapo jana kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo.Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Masasi Fortunatus Mathew Kagoro na kushoto kwake ni Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Masasi diwani wa kata ya Temeke Mh:Uledi Nivako.

 OFISA Rasilimali watu wa Halmashauri ya mji wa Masasi Gresha Sanga wakati anawasilisha Taarifa rasmi kwa Baraza la madiwani ya kuvunja baraza hilo kupisha uchaguzi mkuu ujao utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
 MKURUGENZI wa Halmashauri ya mji wa Masasi Fortunatus Kagoro akizungumza wakati wa mkutano  wa Baraza la Madiwani uliofanyika jana kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo.
 BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya mji wa Masasi ambalo limemaliza muda wake wa miaka mitano na kuvunjwa rasmi jana. Madiwani wakiwa kwenye picha ya pamoja.
 WAHESHIMIWA Madiwani waliomaliza muda wao wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa chama cha Mapinduzi pamoja na mwakilishi wa katibu Tawala wa Mkoa (RAS) Pamoja na mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Masasi.
 MADIWANI waliomaliza muda wao wakiwa kwenye picha ya pamoja na wakuu wa idara na Vitengo wa Halmashauri ya mji wa Masasi.
 MADIWANI waliomaliza muda wao wakiwa kwenye picha ya pamoja na Maofisa watendaji wa kata wa Halmashauri ya mji wa Masasi baada ya baraza hilo kuvunjwa rasmi hapo jana.
MWENYEKITI wa Halmashauri ya mji wa Masasi Andrew Mtumusha (Katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Makamu mwenyekiti Mh:Selemani Nivako (Kulia kwake) pamoja na mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Masasi Fortunatus Kagoro (Kushoto kwake) mara baada ya baraza hilo kuvunjwa rasmi hapo jana.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mtazamo Mpya | Designed By FAHARI YA TANZANIA
Back To Top