TANGAZO
NaClarence Chilumba,Nanyumbu.
Mbunge wa Jimbo la Sengerema William
Ngeleja (CCM) amesema wana CCM wenzake pamoja na wajumbe wa Halmashauri kuu ya
Chama hicho watakaoketi kuchagua jina moja la mgombea wa chama hicho wanapaswa
kumpima kwa mambo 15 aliyofanya katika kipindi chake chote cha uongozi ndani ya
serikali akiwa kama waziri wa Nishati na Madini.
Ngeleja ambaye ni miongoni mwa wagombea
urais ndani ya CCM, aliyasema hayo leo wakati anazungumza na wakazi wa wilaya
ya Nanyumbu mkoani Mtwara pamoja na wana CCM waliojitokeza kumdhamini.
Alisema kiongozi bora anapaswa
kupimwa kwa vigezo vya utendaji bora na uliotukuka kazini huku akijinadi kuwa
yeye wakati huo akiwa waziri wa nishati na madini alifanikiwa kufanya mambo
kadhaa ya msingi ndani ya serikali inayoongozwa na chama cha mapinduzi ikiwemo
uanzishwaji wa mchakato wa ujenzi wa Bomba la Gesi lenye urefu wa Kilometa 542
kutoka Mtwara hadi Dar es salaam.
Alisema wakati anateuliwa na Rais
Jakaya Kikwete kuwa waziri wa nishati na madini alikuta nchi ikiwa kwenye
tatizo kubwa la mgao wa umeme ulioathiri shughuli mbalimbali za kiuchumi ambazo
kwa kiasi kikubwa hutegemea nishati ya umeme lakini kwa juhudi zake na wafanyakazi
wa wizara hiyo kwa ujumla walifanikiwa kumaliza tatizo hilo mnamo mwaka 2011.
Kwa Mujibu wa mtia nia huyo wa chama
cha mapinduzi alisema katika kipindi chake cha uongozi akiwa waziri wa wizara
ya nishati na madini pia walifanikiwa kubuni mradi mkubwa wa umeme vijijini-REA
uliokuwa na lengo la kusambaza umeme kwenye vijiji vyote nchini ili watanzania
wanufaike na matunda ya nchi yao.
“Nimefanya mambo mengi sana ndani ya
nchi hii nikiwa pale wizara ya nishati na madini…si rahisi kuzungumza mambo yote
lakini ukweli ni kwamba wana CCM wanapaswa kuwapima watia nia wa kiti cha urais
kwa vigezo na nadhani kwa sasa William Mganga Ngeleja anafaa kuwa Rais wa Jamhuri
ya muungano wa Tanzania”.alisema Ngeleja.
Alisema masuala mengine aliyofanya ni
pamoja na kudhibiti uchakachuaji wa mafuta uliokuwa unafanywa na baadhi ya
wafanyabiashara wasio waaminifu,kutoa bei elekezi na bei ya kikomo ya mafuta
nchini pamoja na kukarabati miundo mbinu ya shirika la umeme Tanzania (TANESCO)
ambayo mingi ya hiyo ilikuwa katika hali mbaya.
Aidha Ngeleja ameendelea kusisitiza
vipaombele vyake vinne andapo atapewa ridhaa ya kuwa mgombea wa chama cha
mapinduzi na hatimaye kushinda na kuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania
kuwa ni ujenzi wa uchumi imara,uimarishaji wa utawala bora,uimarishaji wa
huduma za jamii pamoja na ujenzi wa miundo mbinu bora.
Akizungumzia kuhusu vijana Ngeleja
alisema anatambua umuhimu wa kundi hilo na kwamba akipewa madaraka na kuwa Rais
atahakikisha analipa kipaombele kundi hilo katika kuendeleza juhudi
zinazofanywa na vijana hao kupitia sera ya mfuko wa vijana.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD