TANGAZO
NA FATUMA MAUMBA, LINDI
KATIKA kutekeleza agizo la Rais Kikwete la kutaka kila
Halmashauri nchini kujenga vyumba vitatu vya maabara kwa ajili ya masomo ya
sayansi katika shule za sekondari za serikali ili kuweza kupata wataalam
wa masomo hayo, Mfuko wa Pensheni wa PSPF mkoani Lindi, wametoa msaada
wa mifuko 300 ya saruji yenye thamani ya shilingi milioni 4.5 kwa ajili ya
kukamilisha ujenzi wa maabara sehemu iliyobakia.
Akipokea msaada huo, Kaimu mkuu wa Mkoa wa Lindi, ambaye pia ni
Mkuu wa wilaya ya Lindi, Yahaya Nawanda, ameushuruku mfuko huo kwa msaada
waliopatiwa kwani utasaidia kukamilisha ujenzi wa maabara kwa shule za
sekondari mkoani humo.
“Mimi nashukuru sana kwa msaada huu wa mifuko 300 ya saruji
utatufanya sasa katika halmashauri yetu ya Lindi kuweza kumaliza kabisa ujenzi
wa maabara kwani hadi sasa hivi imefika zaidi asilimia 90 na Manispaa ni
asilimia mia moja wamemaliza, Manispaa hakuna shida kuhusu maabara
tumemaliza…ila Lindi Vijijini kulikuwa na changamoto nyingi kwani kuna shule
nyingi sana kupitia huu msaada tunaweza kumalizia sehemu iliyobakia.
Hata hivyo Nawanda, aliwataka wananchi wa Lindi pamoja na walimu
wapya ambao wanakuja kuanza kazi mkoa huo pamoja na watu wengine kuona umuhimu
wa kujiunga na Mfuko wa Pansheni wa PSPF ili waweze kujiwekea dhamana yao ya
baadae.
Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF –
LINDI, Ramadhani Mtumwa (Kushoto) akikabidhi Msaada wa Mifuko ya 300 ya Saruji kwa Kaimu Mkuu
wa Mkoa wa Lindi, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Yahaya Nawanda. (Picha
na Fatuma Maumba).
Kwa upande wake Meneja wa PSPF Mkoa wa Lindi, Ramadhan
Mtumwa, alisema wao kama PSPF mkoa wa Lindi, walipata taarifa kuhusu suala la
ujenzi wa maabara kuwa kuna baadhi ya
maabara hazijakamilika kwa wakati kutokana na upungufu wa saruji ndipo
walipoamua kusaidia katika sekta hiyo ya elimu ili kuweza kutoa wasomi wa
masomo ya sayansi ambao watakuja kusaidia nchi yao baadae.
“Sisi PSPF mkoa wa Lindi tulipata taarifa katika suala la ujenzi
la maabara, katika Mkoa wa Lindi kuna baadhi ya maabara ambazo hazijakamilika
lakini zina upungufu mkubwa wa saruji…PSPF kupitia ofisi yake ya mkoa imetoa
mifuko 300 kwa ajili ya ujenzi wa maabara.
Aidha Meneja huyo, amewaomba wadau mbalimbali ambao
wamejiunga na mfuko huo wasisite kusema ni kitu gani kilicho bora na kizuri katika
mfuko huo ili PSPF izidi kuendelea vizuri na iweze kuwepo na kwamba wanapokea
maoni kutoka kwa wateja wao na watayafanyia kazi.
Mifuko 300 ya saruji iliyotolewa na PSPF mkoani Lindi ili kuweza
kumalizia ujenzi wa maabara hizo za masomo ya kemia, fizikia, na baiolojia,
wanatimiza ahadi waliyomwaidi Mbunge wa Viti maalumu Lindi Vijijini, Lulida
Riziki.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD