TANGAZO
Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Mtwara Kassim Bingwe. |
MWENYEKITI wa chama cha
Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Kassim Bingwe hii leo ametangaza rasmi nia
yake ya kugombea nafasi ya ubunge jimbo la Masasi endapo atapewa ridhaa kutoka
kwa UKAWA.
Akitangaza nia hiyo
alisema lengo lake la kugombea nafasi hiyo ni kuleta maendeleo jimbo la Masasi
ambalo alidai kuwa limekuwa nyuma kwa muda mrefu sasa.
Alisema haoni ni kwa
nini kwa sasa wananchi wa jimbo la Masasi wasimpe ushindi ili aweze kuwahudumia
ipasavyo katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Aidha Bingwe
alitangaza pia nia yake ya kugombea nafasi ya udiwani kata ya Mtandi
Halmashauri ya mji wa Masasi.
MWENYEKITI wa CHADEMA mkoa wa Mtwara Kassim Bingwe wakati anatangaza nia ya kugombea nafasi ya Ubunge jimbo la Masasi na udiwani kata ya Mtandi hii leo kwenye viwanja vya mti Mwiba mjini Masasi.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD