TANGAZO
Mkuu wa wilaya ya Ruangwa Mariam Mtima. |
Na Bashiru
Kauchumbe,Ruangwa.
Mkuu wa Wilaya
ya Ruangwa mkoani Lindi Mariam Mtima
amewaondoa hofu ya kutolipwa fidia wananchi waishio kwenye eneo la uwekezaji la Mgodi wa Madini ya Kinywe
(Graphite) kwa kuwa serikali ya wilaya iko kwa ajili ya kutetea wananchi wake.
Alitoa Kauli hiyo jana wakati wa mkutano uliowashirikisha wananchi wapatao 600
ambao mradi huo utachukua maeneo yao kutoka katika vijiji vya Chunyu,Namikulo,Matambalare
Kusini na Kaskazini,Mbekenyera,Namkatila pamoja na kijiji cha Chiundu.
Alisema
Serikali itasimama imara ili kuhakikisha kuwa hakuna mwananchi yeyote ambae
eneo lake au mali yake itachukuliwa na Kampuni ya URANEX ambayo inatarajia kuwekeza
mgodi wa madini ya Kinywe katika vijiji
hivyo pasipo kulipwa fidia.
Alisema ofisi yake tahakikisha taratibu zote
na sheria zinafuatwa katika mchakato mzima wa kulipa fidia kwa watakaoathirika
na ujenzi wa mradi huo wilayani humo na kwamba wataalamu wa uthamini mali na
wataalamu wa sheria kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Lindi watahusika kikamilifu
katika suala zima la ulipwaji wa fidia hizo.
Kwa mujibu wa
mkuu huyo wa wilaya ya Ruangwa alisema wananchi waachane na maneno ya mitaani
ambayo yanapotosha ukweli wa jambo hilo huku wengine wakidai kuwa bei ya
mkorosho mmoja ni kubwa kitu ambacho amekiri hakina ukweli wowote.
kwa upande wake
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa Iss Libaba alisema hakuna jambo lolote litakalofanyika katika
hatua ya uzalishaji wa madini pasipo kulipwa Fidia.
Aidha
alisisitiza kuwa atakuwa bega kwa bega
kuhakikisha kuwa Kampuni ya URANEX inajenga miundombinu bora ya Barabara na
huduma za Jamii katika sekta za elimu,afya,maji ,umeme na mawasiliano ya simu
ili jamii inufaike na uwekezaji huo.
Nae mtaalamu
mshauri kutoka Kampuni ya MTL John Tindyebwa alisema Kwa sasa Kampuni ya URANEX iko katika hatua
ya awali katika mchakato wa kufikia hatua ya ulipaji fidia ambapo kazi ya uthaminishaji mali na ardhi itaanza Julai
mwaka huu na itaishia mwezi Agosti 2015.
Alisema hatua
zingine za kuandaa taarifa ya tathimini ya mali itawasilishwa kwa wananchi
waathirika wapatao 600 ambao mali na ardhi yao vitakuwa vimechukuliwa ili
kupisha ujenzi huo.
Kwa mujibu wa
Tindyebwa kampuni ya MTL inafanya tathimini ya athari za uchafuzi wa mazingira
ambapo taarifa yake itawasilishwa wizara ya nishati na madini ambayo itatoa kauli ya
aidha kuikubali au kuikataa kutegemeana na madhara au kutokuwa na
madhara katika mgodi huo wa madini ya kinywe.
Aidha amewaomba wananchi hao ambao maeneo yao yatachukuliwa
kupisha uwekezaji huo kuondoa hofu kwani hatua ya kuchukua maeneo yao itafikia
mpaka pale tu Kampuni ya URANEX itakapo pata leseni ya uchimbaji.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi ambao maeneo yao
yatachukuliwa kupisha uwekezaji huo Mohamed Mtola aliiomba Ofisi ya mkurugenzi
mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kwa kushirikiana na ofisi ya mkuu
wa wilaya ya Ruangwa kuwasimamia ili kuhakikisha kuwa haki na masilahi yao yanapatikana
pasipo kupindishwa kwa sheria.
Mwisho.
WAJUMBE wa Kamati ya usimamizi iliyoundwa na
wajumbe wawili kutoka katika kila kijiji kati ya vijiji ambavyo mradi wa Mgodi wa
Madini ya Kinywe utatekelezwa wajumbe hao wataungana na kamati ya Wilaya yenye
jukumu la kuhakikisha haki inatendeka kila upande.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Issa Libaba akitoa msisitizo wa jambo katika mkutano huo wa Madini wa
Kampuni ya URANEX pamoja na wananchi wa eneo ambalo mgodi utajengwa wilayani humo.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD