TANGAZO
Watia nia wa Udiwani Masasi kupitia CHADEMA. |
CHAMA cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA) wilayani Masasi hii leo kimetangaza rasmi majina ya
watia nia wake wa nafasi mbalimbali zikiwemo za ubunge na zile za udiwani
wagombea watakaoshindanishwa kwenye mkutano wa UKAWA.
Watia nia waliotangazwa hii leo na chama hicho kwa
nafasi ya udiwani kwa kata ya Nyasa ni
pamoja na Mussa Said Johns,Mussa Mwadewa na Shangwe Omari Manzi,mtia nia mwingine
wa nafasi ya udiwani kwa kata ya Mtandi ni Ebert Johson Mandoa,Kata ya
Mkomaindo ni Said Khatau.
Wengine ni pamoja na
Hassan Bakari Pangara aliyetia nia kwa nafasi ya udiwani kata ya Matawale,ambapo
Moses Chiwinga na Ahmad Ally Namtyoka wakitia
nia kugombea udiwani kata ya Napupa.
Wagombea waliotia nia
kugombea udiwani wa viti maalumu wanawake kupitia Chadema ni pamoja na Sara
Johson Mkwatia pamoja na Mwajuma Rashid.
Wakizungumza baada ya
kutangaza nia wote waliweka wazi vipaombele vyao endapo watapewa ridhaa ya
kugombea kutoka kwa wanachama wa UKAWA na kwamba wako tayari kumuunga mkono
mgombea kutoka kwenye chama chochote kinachounda umoja huo wilayani hapa.
Kwa upande wa nafasi
ya ubunge chama cha CHADEMA kimemtangaza rasmi Mwenyekiti wa mkoa wa Mtwara wa
chama hicho Kassim Bingwe kuwa mtia nia wa nafasi hiyo ya ubunge huku mwingine
aliyetia nia hiyo ni mwalimu Mustapha Swalehe ambaye kwa sasa yuko chuoni
Mtwara.
Hata hivyo Kassim Bingwe aliweka wazi kuwa anatia nia kwa nafasi mbili ikiwemo ya udiwani katika kata ya Mtandi.
WATIA nia wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa nafasi ya Udiwani waliotangazwa leo kutoka kulia ni Sara Johson Mkwatia viti maalumu,Mussa Mwadewa (Nyasa),Ebert Johson Mandoa (Mtandi),Mussa Said Johns (Nyasa),Hassan Bakari Pangara (Matawale),Moses Chiwinga (Napupa),Ahmad Ally Namtyoka (Napupa) pamoja na Said Khatau (Mkomaindo).
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD