TANGAZO
SERIKALI imesisitiza kuwa gharama ya kuwekewa umeme
kwa wakazi wa maeneo ambayo bomba la gesi linapita ni Sh 27,000 na wala hakuna
mabadiliko.
Kauli hiyo ilitolewa jana mjini hapa na Naibu Waziri
wa Nishati na Madini, Charles Mwijage alipokuwa akijibu swali la nyongeza la
Mbunge wa Masasi, Mariam Kasembe (CCM), aliyehoji kuhusiana na gharama hizo kwa
vile baadhi ya wananchi wanalalamika kwamba wanapewa gharama za juu zaidi,
hivyo kutaka ufafanuzi kama kuna baadhi ya sehemu.
Katika majibu yake Naibu Waziri Mwijage alisema
gharama ya kuunganishiwa umeme ni Sh 27,000, wakati fomu ni Sh 5,500 hivyo
jumla ni Sh 32,500, ambazo ndizo mhusika anapaswa kuzilipa.
Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini wakati huo,
Profesa Sospeter Muhongo wakati akitangaza uamuzi huo alisema Serikali imeamua
kupunguza kwa kiasi kikubwa bei ya kuunganisha umeme majumbani na kufikia Sh
27,000 kwa wanavijiji wanaoishi kwenye maeneo ambayo bomba la gesi linapita,
kauli aliyoitoa Januari mwaka jana.
Alisema katika mikoa mingine gharama za kuunganisha
umeme ni Sh 177,000, lakini kwa mikoa ya Lindi na Mtwara gharama hizo
zilishushwa na kufikia Sh 99,000 na baadaye kuwa Sh 27,000.
Gharama hizo ni maalumu kwa ajili ya wakazi waishio
jirani na bomba hilo linaloanzia Mtwara hadi Dar es Salaam kupitia mikoa ya
Lindi na Pwani.
Katika swali lake la msingi Mbunge Msaba jana, alihoji
kuhusiana na agizo la Rais Jakaya Kikwete la kuvipatia umeme vijiji vyote
vilivyopo kwenye barabara kuu ya Mtwara-Karakata, ambapo Naibu Waziri alisema
ni kweli agizo hilo lipo na majina ya vijiji hivyo yapo Tanesco.
Alivitaja vijiji vilivyofanyiwa tathmini kwa ajili ya
kupatiwa umeme kuwa ni Mkwera 1, Mkwera 2, Mumbaka, Mdenga, Mbaju, Ndanda,
Mumburu, Liputu, Liloya na Sululu.
“Vijiji vya Sululu, Liloya, Mbaju na Ndanda Sokoni,
pamoja na vijiji vya Tuungane, Pangani, Nanditi, Nangose Juu, Namkungwi,
Namkinga, Namatutwe na Chikunja tayari vimetengewa kiasi cha Sh bilioni 1.17
kwa ajili ya kuvipatia umeme katika miradi ya nyongeza.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD