TANGAZO
Na Christopher Lilai,Nachingwea.
JUMLA ya kaya 5,856 kati ya 45,769 zilizopo Halmashauri
ya wilaya Nachingwea mkoani Lindi, zimenufaika na mpango wa Tasaf awamu
ya tatu ya mpango wa kunusuru kaya maskini.
Hayo
yamebainishwa na Mratibu wa Tasaf wilaya ya Nachingwea, Sarah Chiwanga wakati
alipokuwa anazungumza na timu ya waandishi wa habari waliotembelea familia
zinazonufaika na mpango huo
Alisema
mpango huo umegawanyika katika vipengele vitatu ambayo ni ruzuku ya
kawaida,elimu na afya,
“katika
mpango huo wilaya imeweza kuzifikia kaya 5856 ambazo zimefanyiwa
uchambuzi na kutambuliwa kisha kuandikishwa.
Alisema halmashauri ya wilaya Nachingwea
ina jumla ya wakazi 206,754 kaya 45,769 lakini kaya
zilizofanyiwa utambuzi ni chache hali ambayo imesababisha kuleta
changamoto nyingi ikiwemo malalamiko ya baadhi ya familia masikini
kuachwa kutoingizwa kwenye mpango huyo jambo ambalo limesababisha na
afisa na watendaji wa vijiji kuingia kulalamikiwa.
“Pamoja
na kufanikiwa kwa zoezi hilo kumejitokeza malalamiko kwa baadhi ya
wanakaya ,baada ya kaya zao kutotambuliwa kutokana na kuchelewa kutoa
ushirikiano kwa maafisa waliokuwa wanapita kuzitambua kaya hizo” alisema Sara.
Chande
Likoko mtendaji wa vijiji cha Nangoe, alisema mpango huo umenufaisha na kuokoa
kaya masikini kutoka kwenye ugumu wa maisha uliokuwepo hapo awali.
Likoko
alisema miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana kupitia mpango huo, ni pamoja na familia
kupata matibabu kwa kutumia mfuko wa afya wa jamii (CHF),familia
maskini kuwa na mifugo,chakula uhakika na kuendesha familia hasa kusomesha
wanafunzi.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD