TANGAZO
Na Clarence Chilumba,Masasi.
WASIFU Umri: Miaka 41 Elimu: Shahada ya Usimamizi wa
Biashara yaani (Barchelor of Business Administration-BBA-Upper Second-Stemmuco
Mtwara. KAZI:Mwalimu.
Historia
yake:
Mustapha
Ahmad Swalehe ni mwalimu ambaye kwa sasa ni mratibu elimu kata ya Temeke
Halmashauri ya mji wa Masasi mkoani Mtwara. Alizaliwa March 3, 1974 huko
wilayani Newala mkoani Mtwara.
Alianza
elimu katika Shule ya Msingi Karume wilayani Newala kati ya mwaka 1983-1989,
mwaka 1990-1993 alisoma katika Shule ya sekondari iitwayo Newala hukohuko wilayani Newala . Baadaye alijiunga
na chuo cha ualimu Mtwara kati ya mwaka 1994-1996.
Mustapha
alisoma darasa la 13 na 14 (kidato cha tano na sita) katika Shule ya kituo cha
chuo cha ualimu Mtwara, kati ya mwaka 2000-2001.
Kati ya mwaka 2008/2010 Mustapha
alipata stashahada ya uongozi na utawala wa elimu
yaani (Diploma in Education Management and Administration) Adem Bagamoyo.
Mwalimu Mustapha Swalehe alipata elimu
ya shahada ya usimamizi wa Biashara yaani (Barcherol of Business Administration
(BBA-Upper Second) Stemmuco Mtwara kati ya mwaka 2012-2015.
UZOEFU KAZINI.
Mustapha Swalehe alianza kazi katika
utumishi wa umma Julai 01, 1999 akiwa mwalimu wa shule ya msingi Chigugu
Halmashauri ya wilaya ya Masasi mkoani Mtwara.
Aidha katika kipindi chote cha utumishi
wake mwalimu Mustapha Swalehe ameshika nyadhifa mbalimbali ikiwemo mwalimu wa
Taaluma (Academic Master) mwaka 2003 katika shule ya sekondari Chiungutwa wilayani
Masasi.
Mwaka 2004 alikuwa mwalimu kiongozi
katika shule ya msingi Nakarara,Mratibu elimu wa kata ya Mpanyani Halmashauri ya wilaya ya
Masasi mwaka 2010 na mwaka 2012 hadi sasa ni mratibu elimu kata wa kata ya
Temeke,Halmashauri ya mji wa Masasi mkoani Mtwara.
KWA UFUPI:
MWALIMU Mustafa
Swalehe kwa mara ya kwanza katika historia ya maisha yake ametangaza rasmi nia
yake ya kugombea nafasi ya ubunge jimbo
la Masasi kwa tiketi ya UKAWA.(Akitokea chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA).
“Moja ya mambo ya
msingi aliyoyasisitiza wakati anatangaza nia yake ni pamoja na kauli yake ya
kwamba ubunge wa sasa ni wa kisayansi unaojengwa kwa hoja za msingi ambazo
zinapaswa kutekelezwa kwa uhakika na kwa ufanisi wa hali ya juu utakaowaletea
maendeleo wananchi wa jimbo la Masasi huku akiwaomba vijana kufanya maamuzi
magumu katika uchaguzi mkuu ujao kwa nafasi ya ubunge.”
Itaendeleaa...........................
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD