TANGAZO
NaFatuma Maumba,Mtwara.
MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama
cha Mapinduzi CCM, waziri mkuu mstaafu Edward Ngoyayi Lowassa, leo amewasili mkoani
Mtwara kusaka wadhamini huku idadi ya watu waliojitokeza kumdhamini wakiwa
zaidi ya elfu tatu na mia tano na kuvuka malengo.
Akizungumza na mamia ya wananchi
waliojitokeza kwa wingi kwenye viunga vya ofisi ya CCM Wilaya ya Mtwara,
Lowassa aliwashukuru wananchi hao kwa kumdhamini kwa wingi zaidi na kwamba huo
ndio umoja unaotakiwa kujengwa na wana CCM.
Hata hivyo Lowasa alisema nia na
madhumuni ya kugombea urais inatokana na
kuchoshwa na umaskini uliokithiri ndani ya Tanzania nchi ambayo wananchi wake
hawapaswi kulalamika kila siku kutokana na umasikini wa kipato.
Aidha Lowassa aliwataka wananchi wa
Mtwara kuendelea kutunza amani iliyopo kwa sasa kwani siri kubwa ya kuja
wawekezaji inatokana na amani iliyoletwa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi.
Pamoja na mambo mengine katika viwanja hivyo
watu walilipuka kwa shangwe baada ya kuwaona Wamasai wakiingia kwa mbwembwe
zote uwanjani hapo na mara ya kufika walianza kucheza kwa kurukaruka huku wakionesha
furaha wakisherekea kwa kumuunga mkono ndugu yao aliyefika mkoani humo kusaka
wadhamini.
Lowassa baada ya kumaliza kusaka
wadhamini mkoani Mtwara, alielekea mkoani Lindi kuendelea kutafuta wadhamini wengine.
Mwisho.
Mtia nia ya Urais kupitia CCM Edward Lowasa akiteta jambo na mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mtwara Mohamedi Sinani,Lowasa alikuwa mkoani Mtwara kwa lengo la kutafuta wadhamini.
Lowasa akiwahutubia mamia ya wananchi wa Mtwara waliojitokeza kumdhamini
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD