TANGAZO
Na Christopher Lilai,Nachingwea.
HOSPITALI ya wilaya ya Nachingwea,mkoa wa Lindi inakabiliwa na
uhaba mkubwa wa shuka hali inayowafanya baadhi wa wagonjwa kuchukua shuka toka
majumbani na wengine kulala bila
kutandika.
Hayo yamebainishwa leo na muuguzi mfawidhi wa hospitali hiyo,John
Leula alipokuwa anapokea mahitaji mbalimbali zikiwemo shuka kutoka kwa Wafanyakazi
wa shirika la umeme nchini,Tanesco wa wilaya ya Nachingwea.
Leula alisema kuwa hospitali hiyo kwa sasa inakabiliwa
na ongezeko la wagonjwa ambao wanatoka nje ya wilaya huku ikiwa na shuka sitini pekee ambazo hazikidhi kwani
punde zinapohitajika kufuliwa
inalazimika vitanda vingi kukosa shuka.
“Kwa wastani tunahitaji shuka angalau nane kwa kila kitanda lakini
hali halisi haiku hivyo kwani kuna wastani wa shuka tatu tu hiyo ni hatari sana
kiafya”.alisema Leula.
Alibainisha kuwa tatizo kubwa ni kukosekana kwa fedha
ambapo alidai iwapo wananchi
wangejitokeza kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF) ungesaidia kuendesha
huduma mbalimbali ikiwepo upatikanaji wa vifaa tiba.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo baada ya kufanya usafi
kwenye eneo la hospitali hiyo,meneja wa Tanesco wilaya ya Nachingwea,Josiah Itegeleiza
alisema misaada hiyo imetokana na michango ya watumishi wa shirika hilo ambapo
ililenga kusaidia makundi maalumu na na kudai kuwa utaratibu huo utakuwa wa kila
mwaka.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD