TANGAZO
Christopher Lilai,Lindi.
Chama cha
wananchi, CUF mkoa wa Lindi kimefanya uchaguzi wa kura za maoni wa kuwapata
wagombea ubunge katika majimbo na wilaya hizo huku Jimbo la Kilwa kaskazini
likimpitisha mtoto wa kigogo wa CCM Kingunge Ngombare Mwiru,Vedastus Kingunge
Ngombare kupeperusha bendera ya CUF.
Vedastus alipita
bila kupingwa kwenye jimbo hilo la Kilwa kaskazini ambalo linashikiliwa na
Muhtadha Mangungu wa CCM huku jimbo la Kilwa kusini mbunge wa sasa kupitia CUF,
Selemani Bwege alipata fursa tena ya kutetea nafasi hiyo baada ya kupata kura
129 na kuwashinda,Mohamed Twahili aliyepata kura 7 na Mwinyi Mohamedi aliyepata
kura 6.
Kwenye mkutano
mkuu wa wilaya ya Nachingwea,wajumbe walimchagua Jordani Membe kuwa
mgombea wa kiti cha ubunge ambapo alitapa kura 195 na kumshinda,Shafih Choaji
aliyepata kura 62.
Wilayani Liwale
Zuberi Kuchaula aliibuka kinara kwa kujipatia kura 179 na kuwashinda,Bashiru
Mdiuma aliyepata kura 94,Jamali Lipwata aliyepata kura 58,Ali Ntila alipata
kura 16,Juma Bei kura 15 na Saidi Mkurungule kura 9.
Mbunge wa Lindi
Mjini Salumu Barwan, alipita bila kupingwa ili kutetea nafasi yake kwa
kipindi kingine cha miaka mitano.
Mkutano wa kura
za maoni wilayani Ruangwa, ulimpitisha Danford Kitwana kuwa mgombea wa nafasi hiyo
kwa kupata kura 94 licha ya ushindi huo kupingwa na wajumbe na kusababisha
mshindi huyo kuondolewa ukumbini hapo chini ya ulinzi mkali wa polisi baada ya
baadhi ya wajumbe kutaka kufanya vurugu kwa kile walichodai kuwa ni mgombea wao ambaye ni Omari Makota ndie aliyestahili ushindi huo.
Kitwana aliwashinda
Omari Makota aliyepata kura 60,Fatuma Kalembo aliyepata 58,Abubakari Kondo aliyepata kura 4,Sharifa Mkundapai aliyeambulia kura tatu pekee na Ramadhan Bacho ambaye hakupata kura hata moja.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD