Loading...
ADVERTISE WITH US ON THIS BLOG.CALL +255 714 789 592/ +255 682 997 767/ +255 752 944 022

ALI KIBA AMBWAGA DIAMOND TUZO ZA KTMA 2015,AONDOKA NA TUZO TANO,UKUMBI WARINDIMA KWA SHANGWE

TANGAZO
Na Clarence Chilumba.
HATIMAYE ule ubishi na ushindani mkubwa wa mastaa wa Muziki wa Kizazi Kipya kati ya Diamond na Ali Kiba umefikia tamati katika ukumbi wa Mlimani City.
Alikiba amefanikiwa kumbwaga Rais wa Wasafi Diamond Platinum kwa kujinyakulia Tuzo Tano huku Diamond A.K.A Dangote akiambulia Tuzo mbili pekee.
Tuzo alizojinyakulia Ali Kiba ni pamoja na Mtunzi Bora wa Mwaka Bongo Fleva,Wimbo Bora wa Mwaka-Mwana,Wimbo bora wa Afro Pop- Mwana,Mwimbaji Bora wa Kiume Bongo Fleva pamoja na tuzo ya Mtumbuizaji Bora wa Muziki wa Mwaka wa Kiume.
Kwa upande wa Mpinzani wake wa Jadi Diamond safari hii ameambulia tuzo mbili pekee ikiwemo ile ya Wimbo Bora wa Zouk au Rhumba -Nitampata wapi na Video Bora ya muziki ya Mwaka- Mdogo mdogo.
Wengine waliojinyakulia tuzo katika kinyang'anyiro hiko ni pamoja na Gwiji la muziki wa Taarab nchini Mzee Yusuph aliyeibuka na tuzo za Kikundi Bora cha mwaka Taarab -Jahazi Modern Taarab,Mtunzi Bora wa Mwaka Taarab na tuzo ya Mwimbaji Bora wa Kiume wa Taarab.
Kwa upande wake Isha Mashauzi nae hakuwa nyuma kwani aliweza kujinyakulia tuzo kadhaa katika usiku huo wa kihistoria uliofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City kwa kujinyakulia tuzo mbili zikiwemo zile za Wimbo Bora wa Taarab-Mapenzi Hayana Dhamana na Mwimbaji Bora wa Kike Taarab.
Wengine waliofanikiwa kujinyakulia tuzo hizo za KTMA 2015 ni pamoja  Yamoto Band waliopata tuzo ya  Kikundi Bora cha mwaka Bongo Fleva,Bendi Bora Ya mwaka -Fm Academia wazee wa Ngwasuma,Wimbo bora wa kushirikishwa au kushirikiana -Kiboko yangu Mwana Fa Ft. Ali Kiba huku tuzo ya Heshima ama Hall of Fame ikienda kwa Gwiji la muziki nchini Marehemu Kapteni John Komba.
Tuzo zingine ni hizi hapa ambazo wasanii waliweza kupata ndani ya ukumbi wa Mlimani City Msanii Bora Chipukizi anayeibukia - Baraka Da Prince
Wimbo Bora wenye vionjo vya asili ya Kitanzania Waite-Mrisho Mpoto
Mtayarishaji Bora wa Nyimbo wa Mwaka Bendi-Amoroso
Mtayarishaji Bora wa Nyimbo wa Mwaka Taarab-ENRICO
Mtayarishaji Bora wa Nyimbo wa Mwaka Bongofleva-NAREEL
Mtunzi Bora wa Mwaka Hip Hop-Joh Makini
Mtunzi Bora wa Mwaka Bendi- Jose Mara.
Wimbo Bora wa Afrika Mashariki-Sura yako-Sauti Sol
Msanii Bora wa Hip Hop-Joh Makin
Rapa Bora wa Mwaka Bendi- Ferguson
Wimbo Bora wa Reggae/DanceHall-Let Them Know- Maua Sana
Wimbo Bora wa Hip Hop-Kipi Sijasikia-Profesa Jay Ft. Diamond Platinum
Wimbo Bora wa R&B- Sisikii-Jux
Wimbo Bora wa Kiswahili Band-Wale Wale Vijana Ngwasuma
Mwimbaji Bora wa Kiume Bendi-Jose Mara
Mwimbaji Bora wa Kike Bongo Fleva-Vanessa Mdee
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mtazamo Mpya | Designed By FAHARI YA TANZANIA
Back To Top