TANGAZO
Na Bashiru Kauchumbe,Masasi.
WANAFUNZI wanaounda
jumuiya ya wahitimu waliowahi kusoma katika shule ya Sekondari chidya iliyoko wilayani
Masasi Mkoani Mtwara wameamua kuchangia Fedha shilingi Milioni 2.5 kwa ajili ya ununuzi wa Madawati ili
kuweza kuondoa changamoto ya upungufu wa Madawati katika shule hiyo.
Fedha
zilizochangishwa zinaweza kununua madawati 30 na kwamba tayari kamati ya kusimamia utengenezaji wa madawati hayo imeshaundwa kilichobaki ni utekelezaji wa
suala hilo ambalo ni muhimu katika uboreshaji wa sekta ya elimu nchini.
Akizungumza na Blog
ya Mtazamo Mpya mwenyekiti wa jumuiya hiyo Hasani Abbasi alisema uamuzi wa kuchangisha
fedha hizo ulipitishwa wakati wa mkutano mkuu wa jumuiya hiyo uliofanyika
jijini Dar es salaam mwanzoni mwa mwaka huu
ambapo kila mwanafunzi aliyesoma katika shule ya wavulana ya Chidya anapaswa kuchangia fedha kwa ajili ya
ununuzi wa Madawati hayo.
Alisema utaratibu wa kuchangia michango hiyo upo wazi na kwamba
wanachama wote wameunganishwa kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo WhatsApp na
Facebook hivyo wanachama wote waliounganishwa kwenye mitandao hiyo ni wajibu
wao kuchangia.
Hata hivyo alisema muitikio wa watu kuchangia ni mdogo ukilinganisha na idadi ya watu waliowahi kusoma shule hiyo yenye historia
kubwa nchini huku akitoa wito kwa wanafunzi wote waliosoma shule hiyo kuunga
mkono jitihada za wenzao walioamua kuanzisha utaratibu huo wenye manufaa kwa
shule hiyo.
Alisema katika kufanya
uhamasishaji wa michango hiyo wamekuwa wakikumbana na changamoto mbalimbali
ikiwemo kukatishwa tamaa na baadhi ya
watu waliowahi kusoma shule hiyo kwa
madai kuwa utaratibu huo unalenga kuwanufaisha watu wachache na sio shule na kwamba
mpango huo ni wa kitapeli kitu ambacho si cha kweli.
Shule ya Sekondari chidya ilianzishwa rasmi
mwaka 1923 lakini ipo katika hatari ya kupoteza hadhi yake kwa kuwa kwa
sasa inakabiliwa na changamoto
mbalimbali ikiwemo uchakavu wa majengo,ukosefu wa vitanda pamoja na madawati
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD